Serikali inapaswa kulinda na kudumisha haki msingi za raia wake ili kuendeleza amani
na utulivu!
Askofu mkuu Paul Ruzoka, Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Amani, Baraza la Maaskofu Katoliki
Tanzania katika mahojiano na Radio Vatican anabainisha kwamba, mchakato wa majadiliano
ya kidini katika kujenga, kulinda na kudumisha misingi ya haki, amani na utulivu nchini
Tanzania unapaswa kusimamiwa vyema na Serikali yenyewe.
Askofu Ruzoka
anasema kwamba, shida kubwa inayojitokeza kwa sasa ni kuangalia masuala mbali mbali
ya uvunjifu wa misingi ya haki na amani kama kielelezo cha kinzani na misigano ya
kidini nchini Tanzania, jambo ambali si kweli. Haki msingi za raia na usalama wa maisha
ya raia na mali zao ni mambo yanayopaswa kupewa msukumo wa pekee na Serikali ili kudumisha
misingi ua uatwala bora kwa kuhakikisha kwamba, haki ya kila raia inalindwa na amani
ina tawala.
Masuala ya uvunjifu wa amani yaangaliwe zaidi katika misingi ya
haki na kwamba, haki isipolindwa na kudumishwa kunaweza kutokea uvunjifu wa amani.