2013-06-10 14:26:48

Mh. Padre Jeremiah Madimetja Masela ateuliwa na Papa kuwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki Polokwane, Afrika ya Kusini!


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Jeremiah Madimetja Masela kutoka Jimbo Katoliki la Polokwane, Afrika ya Kusini kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Polokwane, Kabla ya uteuzi huu Askofu mteule alikuwa ni Msimamizi wa kitume wa Jimbo Katoliki Polokwane. Alizaliwa tarehe 28 Juni 1958 mjini Polakwane. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikuhani, akapadrishwa hapo tarehe 15 Desemba 1984.

Katika maisha yake kama Padre amewahi kuwa Paroko msaidizi, Makamu wa Askofu Jimbo Katoliki Polokwane, Padre wa maisha ya kiroho, Seminari kuu ya Mt. Yohane Vianney iliyoko mjini Pretoria. Baadaye aliteuliwa tena kuwa Makamu wa Askofu na Paroko na kuanzia Mwaka 2011 aliteuliwa kuwa ni Msimamizi wa Kitume, Jimbo Katoliki Polokwane, ililokuwa wazi baada ya Askofu Mogale Paul Nkhumishe kung'atuka kutoka madarakani Desemba 2011.







All the contents on this site are copyrighted ©.