Mchango wa vyombo vya habari vya kikristo katika kuhamasisha haki, amani, upatanisho
na haki Mashariki ya Kati
Warsha ya siku mbili iliyojadili kuhusu mchango wa vyombo vya habari vya Kikristo
katika nchi za Kiarabu imehitimishwa hivi karibuni kwa kupewa changamoto ya kuendelea
kutoa huduma ya haki, amani, upatanisho na haki msingi za binadamu. Warsha hii imehudhuriwa
na viongozi mbali mbali wa Makanisa kutoka Mashariki ya kati na Askofu mkuu Claudio
Maria Celli, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Jamii alihudhuria pia.
Wajumbe
kwa pamoja wameangalia mchango makini uliotolewa na vyombo vya habari vya kikristo
katika mapambazuko ya mapinduzi ya Kiarabu na kwamba, bado kuna changamoto kubwa kwa
waamini wa dini mbali mbali huko Mashariki ya kati kuishi kwa amani na utulivu; kwa
kuheshimiana na kuthaminiana kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wengi.