2013-06-10 14:46:06

Mashirika ya Kipapa ya Kazi za Kimissionari Kenya na Algeria yapata wakurugenzi wapya


Kardinali Fernando Filoni, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu ameridhia uteuzi wa Padre Celestino Bundi kuwa mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa ya Kazi za Kimissionari nchini Kenya kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka 2017.

Wakati huo huo, Kardinali Filoni pia amemteua Padre Mario Cassera kuwa Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa ya Kazi za Kimissionari nchini Algeria kwa kipindi cha miaka mitano, yaani kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2018.







All the contents on this site are copyrighted ©.