Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya 28 ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2013 yanazidi
kupamba moto huko Rio de Janeiro, Brazil. Kamati ya Maandalizi inabainisha kwamba,
tayari kuna vituo 273 ambavyo vimeandaliwa rasmi kwa ajili ya katekesi na vipindi
vya sala. Kutokana na idadi kubwa ya vijana wanaotarajiwa kushiriki, vijana hao watapaswa
kukusanyika kwenye: makanisa, kumbi na viwanja wa michezo ndani ya Jimbo kuu la Rio
de Janeiro pamoja na majimbo ya jirani.
Maeneo yote yamebahatika kuwa na Katekesi
itakayotolewa kwa lugha ya Kireno na Kihispania. Kuna vituo 25 vilivyopangwa kwa ajili
ya katekesi kwa lugha ya Kiingereza, Kiitalia na Kifaransa. Kuna maeneo 8 yatakayotoa
katekesi kwa lugha ya Kijerumani na vituo 5 kwa ajili ya lugha ya Kipoland. Vijana
watasindikizwa kwenye vituo vya katekesi karibu na maeneo watakapokuwa wamefikia.
Kwa mahujaji ambao watakuwa na ulemavu, wao wamepangiwa sehemu moja maalum na wote
watakusanyika hapa na kutakuwa na watu watakaofanya tafsiri hapo kwa papo!.