2013-06-07 07:27:05

Siku kuu ya Moyo Mtakatifu wa Yesu; waombeeni Mapadre wenu!


Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kumshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha na miito ya Kipadre. Anawataka kuwasindikiza Mapadre wao kwa njia ya sala, wema na ushauri mzuri. Baba Mtakatifu ameyasema hayo wakati alipokuwa anawapongeza Mapadre wapya kutoka Poland walioshiriki katika Katekesi yake kwa siku ya jumatano aliyokazia kwa namna ya pekee umuhimu wa utunzaji wa mazingira na hifadhi kwa binadamu.

Katika Siku kuu ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, Baba Mtakatifu anawaalika Mapadre kumshukuru Mungu kwa zawadi na maisha ya Kipadre. Anawaalika kwa namna ya pekee kukuza ndani mwao mwanga na nguvu ya Roho Mtakatifu, ili waweze kumtumikia Mungu na jirani zao kwa ari na moyo mkuu, daima wakichuchumilia utakatifu wa maisha.









All the contents on this site are copyrighted ©.