Papa aasa utume wa kidiplomasia si ajira bali ni utumishi
Baba Mtakatifu Fransisko, Alhamisi alizungumza na mapadre wanafunzi katika aasisi
ya Elimu ya Kikanisa, ambayo hujishughulisha mafunzo kwa Mapadre walio chaguliwa
kuingia katika utume wa ofisi za Kidiplomasia za Kibalozi na katika Sekretarieti ya
Jimbo la Takatifu.
Katika hotuba yake, Baba Mtakatifu aliwakumbusha Mapadre
wanafunzi kwamba ni lazima wapandikize kwa kina maisha ya kiroho kwa ajii ya kuweza
kupata uhuru wa ndani,ambacho ni kigezo muhimu kwa kazi yao ya baadaye. Pia alionya
dhidi ya tamaa za kutaka kupanda madaraja , akishutumu kwa mara ingine, kuuchukulia
utume huu kama vile ni ajira, akiuita moyo wa namna hiyo kuwa sawa na ukoma.
Papa
Francis alitoa maelezo yake kwa kutazama sana mfano wa maisha ya Mwenye Heri Papa
Yohane XXIII, akisema ni mfano wa kuigwa na wale wanaotaka kuwa wanadiplomasia. Papa
pia alitoa shukurani za kipekee maalum kwa Masista wote wanaofanyakazi katika Chuo
hiki cha Kipapa, kwa huduma yao nzuri na majitoleo na upendo wao, katika kumtumikia
Bwana.
MwishoPapa aliomba sala za mapadre kwa ajili yake mwenyewe na aliwakabidhi
katika ulinzi wa Mama Bikira Maria na kwa Mtakatifu Anthony Abbate msimamizi wao.
Na aliwahakikishia sala na baraka zake, wakati wote wa majiundo yao.