2013-06-07 11:29:57

Padre Fernando Domingues ateuliwa kuwa Katibu mkuu Shirika la Kipapa la Mtakatifu Petro


Kardinali Fernando Filoni, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu, amemteua Mheshimiwa Padre Fernando Domingues kuwa katibu mkuu wa Shirika la Kipapa la Mtakatifu Petro ambalo linajihusisha kikamilifu kwa ajili ya majiundo ya Mapadre mahalia na kwa sasa linajihusisha pia na majiundo ya Majandokasisi katika nchi za Kimissionari.

Padre Fernando Domingues mwenye umri wa miaka 54 hadi kuteuliwa kwake alikuwa ni Gombera wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana kuanzia mwaka 2005.







All the contents on this site are copyrighted ©.