2013-06-07 08:57:40

Italia yachanga kiasi cha Euro millioni 6 katika miradi ya kilimo


Serikali ya Italia imesema kwamba, itachangia kiasi cha Euro millioni 6 kwa ajili ya kuendeleza mikakati ya maboresho ya sekta ya kilimo inayotekelezwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO. Italia inagharimia miradi ya kilimo ipatayo 50 kwa kiasi cha dolla za Kimarekani millioni 127.2.

Italia ni kati ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika mikakati ya maboresho ya sekta ya kilimo duniani. Mkazo mkubwa kwa sasa unaelekezwa katika harakati za kuhakikisha kwamba, kuna uhakika na usalama wa chakula duniani, jambo ambalo linavaliwa njuga na Italia kwa kushirikiana na FAO. Asilimia 40 ya fedha zote zinazotolewa na Italia zinagharimia miradi ya kilimo Kusini mwa Jangwa la Sahara.







All the contents on this site are copyrighted ©.