2013-06-06 15:06:27

Papa anaomboleza kifo cha Kardinali Stanislas Nagy


Kardinali Nagy Stanislaus wa Poland alifariki dunia umatano. Kwa kifo chake , idadi ya Makadinali sasa ni 205 ambao kati yao 113 ni wapiga kura katika conclave na 92 hawana haki hiyo.
Papa Fransisko mara baada ya kupewa taarifa za msiba huu, alituma salaam za rambiirambi kwa njia ya telegram kwa Kardinali Stanislaw Dziwisz, Askofu Mkuu wa Krakow, ambamo ameonyesha masikitiko na mshikamano wake kwa wote walioguswa na msiba huu.

Kardinali Nagy Stanislas, SCI, alikuwa mwanashirika wa Mapadre wa Shirika la Moyo Mtakatifu wa Yesu (Dehonians), alizaliwa tarehe 30 Septemba 1921, Bieruń Stary, Jimbo Kuu la Katowice (Poland). Yeye aliingia Usharika wa Mapadre wa Dehonian ,mwaka 1937. Na Julai 8, 1945 aliyeteuliwa Mkuu wa Shirika.

Pia aliwahi kuwa Gombera wa Seminari Ndogo ya Mapadre wa'Dehonian ya Kraków-Płaszów na baadaye Seminari Kuu ya shirika iliyoko Tarnów. Na alifundisha katika Chuo Kikuu Katoliki ya Lublin ambapo, mwaka 1972, akawa Profesa kamili.

Salaam za ranbirambi za Papa kwa Kardinali Stanislaw Diswisz, zimeonyesha mshikamano wa kiroho kwake yeye na jumuya nzima na kwa familia ya kiroho ya marehemu, na Usharika wa Mapadre wa Dehonian na wote wanaoomboleza msiba huu. .
Papa Fransisko kwa upendo wadhati amekumbuka fadhili na wema wa Marehamu kwa Kanisa, hasa katika dunia ya wasomi, ambamo yeye alipenda daima kujiendeleza hara akaweza kuwa m,somi mtalaam wa teolojia na hasa nidhamu za kiteolojia. Na pia amekumbuka ushirikiano wake mkubwa uliowezesha kuzaa matunda ya urafiki wa karibu na Mwenye Heri Yohane Paulo II, na pia kwa ajili ya utendaji wa pamoja katika shughuli za kiekumene.
Kwa moyo wa dhati Papa anatolea sala zake kwa Bwana, kupitia maombezi ya Bikira Maria, apate kumkabariki mtumishi wake mwaminifu, na mtu mashuhuri wa Kanisa, katika furaha na amani milele. Papa pia anaomba faraja na neema za Kristu Mfufuka ziwashukie waombolezaji wote.








All the contents on this site are copyrighted ©.