Papa Fransisko anawaonya Wakristu, kujiweka mbali na lugha ya unafiki kwa kuwa unafiki
huweza kuonyesha kama vile yote ni haki, lakini kumbe ni sababu za uongo. Na hivyo
Mkristo anapoitanganza Injili, hapaswi kutumia lugha ya kinafiki , lakini kusema
ukweli wa Injili na uwazi kama asemavyo mtoto mdogo. Na kwamba “Hakuna ukweli bila
ya upendo, maana upendo ni Ukweli”. Ni mafundisho ya Papa Fransisko wakati ya Ibada
ya Misa siku ya Jumanne, aliyoiongoza katika katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta
la ndani ya Vatican.
Papa baada ya kuzungumzia juu ya ukana Mungu siku ya
Jumatatu, Jumanne aliendelea kuitazama lugha ya wanafiki, akiangalisha katika somo
la Injili ya siku: lililo lenga katika malipo ya kodi ya Kaisari, na Mafarisayo na
Waherodiani, wakimhoji Yesu kwa hila, juu ya uhalali wa kodi hiyo.
Papa Fransisko
alibainisha nia na mbinu ya mafarisayo ya kumtega Yesu kwa hila, iliajibu tofauti
nayale anayoyahubiri , swali kama ni halali au si halali kulipa kodi kwa Kaisari,
tena waliuliza kwa ugha laini, na maneno mazuri, huku wakijionyesha kama ni marafiki,
na kumbe ni wanafiki. Ndani mwao, hawana ukweli, ila uongo na unafiki , wakijifunika
kwa lugha nzuri ya uongo. Lugha ya kulaghai na kuwajaribu wengine kwa hila, majaribu
ya kuwaangusha kiimani kupitia ujanja wa lungha danganyifu na uongo. Wao wana mioyo
ya uongo, isiyo kuwa na ukweli.
Papa ameiita lugha hii ya kinafiki kwamba
haina tofautina ukani Mungu. Yesu aliwaasa wanafunzi wake wajiepushe na lugha hiyo,
bali wausimamie ukweli ambao ni upendo. Unafiki lugha ya ukweli maana ukweli daima
hujitenga na uongo. Hakuna ukweli bila upendo . Kama hakuna upendo , hakuna pia
ukweli. Na kwamba daima wanafiki wanataka ukweli uliofungamanishwa na maslahi yao
kwa mbinu nyingi tofauti tofauti kama ubinafsi, miungu ya unyonyaji a kutaka kunufaika
toka kwa wengine, wenye kuwaongoza katika kuwasaliti wengine na wenye kuwaongoza
katika madhulumu na unyanyasaji wa uaminifu.
Papa Francis iliendelea, kuzungumuzia
lugha hii ya kinafiki kwamba imejaa radha ya kejeli na uongo, kama ilivyokuwa Siku
ya Alhamis Kuu, walipomtuhumu Yesu na kumkamana na kumpeleka kwa Pilato , siku ya
Ijumaa, Yesu aliutetea ukweli hadi msalabani, bila ya lugha ya kinafiki. Ndivyo
Yesu anavyowataka wafuasi wake wawe. Kusimamia ukweli katika hali zote, kama alivyo
mtoto mdogo . Papa alikamilisha homilia yake kwa kumwomba Bwana, ili kwamba leo
hii lugha ya wafuasi wake iwe ni lugha nyepesi , lugha yenye ukweli kama wa mtoto
mdogo, ambayo ni lugha ya kimungu na lugha ya ukweli katika upendo.