2013-06-05 15:32:17

Papa - imarisheni mapambano dhidi ya utamaduni wa uharibifu


Katekesi ya Papa , yasisitiza uimarishaji wa mapambano dhidi ya utamaduni wa Uharibifu unao amrishwa na fedha na si binadamu.
Papa Fransisko alisisitiza katika Katekesi yake yake ya Jumatano hii, iliyohudhuria na umati mkubwa wa watu waliofurika ktika uwanjawa Kanisa Kuu la Mtaktifu Petro, tangu mapema asubuhi.
Papa alitazamisha Katekesi yake zaidi kaitka maana ya uwepo wa adhimisho la Siku ya Mazingira duniani , inayofanikisha na juhudi za Umoja wa Mataifa, kwa ajili ya kutoa angalisho na himizo zaidi, katika haja ya kufuta uharibifu wa chakula duniani kama moja ya kigezo muhimu katika kupunguza tatizo la njaa duniani.
Papa aliuambia umati mkubwa wa wamahujaji na wageni kwamba, anapozungumzia juu ya mazingira na viumbe, mawazo yake moja kwa moja anaya peleka katika kurasa za Kitabu cha Mwanzo cha Biblia, ambamo imeandikwa, Mungu, alimweka mwanamume na mwanamke katika bustani ya edeni ailime na kuitunza aridhi (taz. Mwanzo 2 , 15).
Maelezo ya Papa , yamehoji , iwapo binadamu wa kisasa anaelewa maana ya kulima na kuitunza aridhi, na iwapo anawajibika katika kuitunza aridhi na viumbe wake , au ndiyo amekuwa mharibifu mkubwa wa aridhi na viumbe vyake.
Alifafanua kuilima aridhi, daima ni kuihudumia aridhi , kwa sababu huduma hiyo huzalisha matunda, ingawa kiasi kinacho zalishwa hutegemea na mkulima anavyojituma. Na kwamba, kulima na kutunza viumbe ni sharti lililotolewa na Mungu, tangu mwanzo wa kuumbwa dunia , si tu kwa ajili ya kundi fulani la watu lakini kila mmoja wetu anayo sehemu yake, katika wajibu wa kufanikisha urutubishaji wa aridhi na kuigeuza kuwa bustani nzuri na mahali panapofaa kwa kila mmoja kuishi vyema.
Na kwamba, Papa Mstaafu Benedict XVI, mara kwa mara alikumbusha kwamba, kazi hii tuliyokabidhiwa kwetu na Mungu Muumba, inahitaji kufahamu mwenendo wake na mantiki ya viumbe. Lakini mara nyingi sisi tunaendeshwa shughuli zetu na kiburi cha mamlaka, halala za kutaka mali na faida zisizokuwa na kiasi, na hivyo kutokuwa tena walinzi waliopewa dhamana ya kuitunza, kuilinda na kuihudumia aridhi , iliyotolewa kama zawadi ya bure, badala yake tunakuwa waharibifu wasiofaa kitu.
Papa alieleza na kutoa wito kwa watu wote, kutopoteza dhamana hii ya kuilinda aridhi na viumbe wake, huku akihimiza kwa mara nyingine, kusoma na kutafakari kile Benedict XVI alicho elezea juu ya upendo wa kati ya Mungu na mwanadamu. Papa alihoji, kwa nini uharibifu huu unatendelea kutokea?Na kwa nini tunahisia za kutaka kuishi kinyume na kujiweka mbali na maongozi ya Mungu, na hata bila ya kusoma ishara zake?

Kisha aliendelea kuainisha uhusiano huo kwamba, si tu kati ya binadamu na mazingira, kati ya mtu na viumbe, lakini pia kuhusu mahusiano kati ya binadamu na binadamu . Na aliizungumzia kwa kirefu juu ya ekolojia ya binadamu, uhusiano wa karibu na ikolojia ya mazingira, akisema , wakati huu ambamo tunaishi wakati wa mgumu wa migogoro ya mabadiliko ya abia nchi na mazingira, hasa kwa sababu zinazoletwa na utendaji mbovuwa binadamu , basi binadamu kiumbe hatari kwa mazingira . Ni binadamu yuleyule aliyepewa dhamana ya kutunza,kulinda na kuyahudumia mazingira , anageka na kuwa hatari, kwa vile alivyokabidhiwa kuvilinda. Anakuwa hatari si tu kwa sababu za kiuchumi, lakini pia tatizo la maadili na kijamii.

Papa aliendelea kueleza kwamba, Kanisa kwa mara kadhaa, limesisitiza, kutendea haki mazingira na wengi huitikia ndiyo, hiyo ni haki, lakini ni kweli tu kwamba ni mwitikio wa ndiyo ya kinafiki ..maana mifumo mbovu dhdi ya mazingira na viumbe inaendelezwa kwa halala za kutaka mafanikio zaidi ya kiuchumi na ukosefu wa maadili katika fedha.

Papa ametaja , leo hii kinacho amrisha si tena binadamu, bali ni fedha: fedha, imeshika hatamu ya uongozi, fedha ndiyo inamrisha, na kusahau kwamba, Mungu, Baba yetu alitupa kazi hii ya kuitunza aridhi ni si fedha.
Papa amehimiza wake kwa waume kulirejea agizo la Mungu la kuitunza aridhi na kuihudumia kwa upendo nakujiweka mbali na mwelekeo wa kumezwa na tamaa za kujilimbikia fedha. Aliwataka wake kwa waume wajitolee mhanga, kuvunja janga la la umaskini, linalosababisha na wachache kuichezea aridhi kwa manufaa yao binafsi.
Aliendelea kulaani utamaduni huu mbovu, unaoshindwa kujua thamani ya maisha ya mtu na kuyalinda hata kama ni maskini au malemavu, kwa kuwa binadamu wote mbele ya Mungu wana heshima sawam hata yule mtoto aliye tumboni,bado, na wale wanaonekana hawana tena msaada wowote katika jamii au kama vile wazee.
Na kwmaba, utamaduni huu mbovu wa ulafi wa mali, unaendelea kugandamiza watu wengi hasa familia maskini zinazosumbuliwa na njaa na utapiamlo. Papa alikumbusha wakati wa mababu zetu walikuwa makini katika suala la kutupa chakula jalalani. Lakini mfumo wa leo wa ulafi wa mali, unasababisha wengi sasa kujilimbikia chakula na kila siku hukitupa jalalani, ziada ambayo,ingeweza kupelekwa kwa wahitaji wengine, hasa waliokabiliwa na majanga asilia kama ukame na mafuriko. Papa amefananisha chakula hicho kinachotupwa na wenye navyo kuwa ni sawa na kumpokonya maskini chakula chake mezani na kukitupa jalalani. ni sawa na kumwibia maskini chakula kutoka meza yake.
Na mwisho wa Katekesi yake, Papaalikutana na vyama na mashirika yanayoshughulikia kipeo cha ubinadamu Syria, kama ilivyoandaliwa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Misaada ya Kibindamu cor Unum.
Alisema mbele ya uso wa ghasia na fujo zinazo endelea Syria, narudia kutoa tena kwa nguvu zote , ombi la kupatikana amani . Na alihimiza juhudi zilizo anzishwa na Jumuiya ya Kimataifa kupata suluhu haraka iwezekanavyo kukomesha uharibifu huo wa maisha na vitu Syria.
Na pia alitoa angalisho kwa jumuiya za Kikristu nchini Syria ,akisema, kanisa liko daima nyuma yao kwa namna ya kipekee. Na kwamba mashirika ya misaada yana wajibu mkubwa katika kudumisha uwepo wa Wakristu katika taifa hilo, mahali walipozaliwa na kukulia Wakristu hao. . Na hivyo ni wajibu wetu pia kuhakikisha mashahidi hawa wa Kristu wanaendelea kuwepo Syria.








All the contents on this site are copyrighted ©.