Jumatatu katika kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya wafia dini wa Uganda , mwaliko
ulitolewa kwa Papa Francis kuitembelea Uganda. Mwaliko huo ulitolewa na Askofu Mkuu
Paul Bakyenga wa Jimbo Kuu la Mbarara, siku ya Jumatatu , wakati akiongoza Ibada
ya Misa kwa nia adhimisho la miaka 125, ya wafiadini wa Uganda. Mwishoni mwa
wiki iliyopita, maelfu ya waaamini walianza kumininika mjini Mbarara, ili Jumatatu
waweze kushiriki katika maadhimisho ya miaka 125 ya Wafia dini wa Uganda. Ibada iliyofanyika
katika Madhabahu ya Namugongo,iliyo anza majira ya saa nne za asubuhi Jumatatu, kuenzi
na kumsifa Mungu kwa ajili ya ushupavu wawafia dini hao.
Wakatoliki wafia
dini wa Uganda waliuawa 1886, kwa amri ya Kabaka Mutesa kwa kuwa walikataa kuikana
imani Katoliki. Kwa heshima yao Madhabahu yamejengwa mahali alipouawa Mtakatifu
Charles Lwanga kwa kuchomwa moto kwa kuwa alikataa kuukana ukatoliki. Taarifa
zinasema, kwa muda wa siku kadhaa kabla ya adhimisho, mahujaji na waaamini walifuata
nyayo za mateso na sulubu walizopitia wafia dini 22 wa Uganda kwa Ibada , tafakari
na mafungo binafsi. Na kwamba tukio zima lilipambwa kwa nyimbo na utamaduni mahalia
wa kabila la Wanyankole .Na mahujaji bila ya kujali ukali wa jua lililokuwa likiwaka
, waliendelea kuimba na kutolea sala, maombi na kumsifu Mungu . Hija hii imetajwa
kuwa iliandaliwa vyema na imependeza na kuwa kivutio kwa watu wengi kushiriki.