Rasimu ya Katiba ya Tanzania kuzinduliwa Jumatatu, Juni 3, 2013
Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania inapenda kuwafahamisha wananchi wote
kuwa itafanya uzinduzi wa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku
ya Jumatatu, Juni 3, 2013, kuanzia saa 8:00 mchana katika viwanja vya Karimjee, jijini
Dar es Salaam. Uzinduzi huo utarushwa moja kwa moja na vituo vya redio vya TBC
Taifa, ZBC Redio na vituo vya televisheni vya TBC 1 na ZBC TV na vituo vinginevyo
vya redio na televisheni. Rasimu hiyo ya Katiba imetokana na maoni ya wananchi,
viongozi na makundi mbalimbali waliyowasilisha kwa Tume kupitia njia mbalimbali zikiwemo
mikutano, barua pepe, ujumbe mfupi wa simu za mikononi (sms) na nyinginezo. Tume
inawaomba wananchi na wadau kufuatilia uzinduzi huo kwa makini kupitia vyombo hivyo
vya habari.