Usafirishaji wa watu kinyume na haki, ni fedheha kubwa isiyoweza kuvumiliwa.
Baba Mtakatifu Fransisko, amelaani vikali uwepo wa mipango ya kusafirisha watu kinyume
na haki za binadamu. Kemeo hilo alilitoa wakati akikutana na wajumbe wa Mkutano Mkuu
wa Baraza kwa ajili ya Huduma za Kichungaji kwa wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi
maalum, ambao wapo Roma kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya Mkutano wa Baraza wa Mwaka
vilivyoanza siku ya Jumatano. Mada kuu ya Mkutano huo ni “Watu waliolazimishwa kuhama
makazi yao”. Baraza linatazama kwa makini kwa jinisi gani Kanisa linaweza kutoa msaada
wa kufaa kwa watu hao. Katika hotuba yake, Papa ameonyesha kujali mwelekeo wa
kukua kwa wimbi la watu kulazimishwa kuhama makazi yao kwa namna mbalimbali na hasa
mipango ya kurubuni watu kwenda maeneo ya mbali na makazi yao kwa muono kwamba wanakopelekwa
watapata ajira na kumbe sivyo. Papa ameiita mipango hiyo haramu ya kusafirisha watu
kwa nia mbovu, kuwa ni fedheha kubwa inayo dharirisha ubinadamu wa mtu. Kwa ajili
yaowatu hawa wanaodharirishwa, Papa ametoa wito kwa mataifa kuchukua hatua za kulinda
utu wa watu hao kama jambo la kidharura. Alisistiza usafirishaji wa watu ni ujinga
na aibu kwa jamii yetu inayojiita imestraabika. Wanyonyaji na wabia wao wote na katika
ngazi zote za biashara hii, wanapaswa kuchunguza kwa makini dhamiri zao wenyewe
na mbele ya Mungu. " Papa amesisitiza, Kanisa kwa mara nyingine, linarudia kutoa
ombi lake kwa nguvu, kwamba ni lazima kutunza na kulinda hadhi na utu wa binadamu.
Na hiyo ina maana ya kuheshima haki za msingi kwa kila binadamu. Ni jambo la aibu
kusikika kuna watu wanaodiriki kuuza wenzao kama vileni bidhaa, katika dunia ambamo
kuna majadiliano mengi ya haki. Inafedhehesha kusikia wtu wanapuuza haki na maazimio
ya Umoja wa Mataifa na kufinyanga haki na utu wa mtu, katika dunia ambamo watu wanazungumza
kuhusu haki. Papa Fransisko analaani utafutaji wa fedha wa namna hiyo kuwa ni
balaa na fedh ainayopatikana ni chafu . Alieleza na kuonyesha kujali kwamba sasa
tunaishi katika dunia ya kujali fedha. Tunaishi katika ulimwengu, na katika utamaduni
wa ufalme wa fedha. Ni lazima kuukataa ufalme huo wa tamaa za kujilimbikia fedha
wenye kufisha heshima ya Utu wa mtu. Ufalme unaopokonya mastahili hasa ya watu wanyonge
na maskini , kuwadharirisha na kuwapuuza. Papa Fransisko ametoa ombi kwa watawala
na wabunge wa kila jumuiya kitaifa na kimataifa, kulitazama jambo hili kwa makini
na kukomesha madhulumu yote. Papa, umezitazama hali halisi ya watu waliolazimishwa
wakiyakimbia makazi yao akisisitiza, mipango madhubuti na mbinu mpya ziandaliwe,
ili kulinda heshima ya wanaokumbana na matatizo hayo na maisha yao yaboreshwe na kupata
msaada katika kukabiliana na changamoto zinazoibuka kutokana njia za kisasa za ukandamizaji
mateso, na utumwa. Papa anawaombea wote walioingizwa katika madhulumu haya makali
, ili waweze kupata nguvu za kurejesha maisha yao kawaida, kwa uvumilivu, saburi
, furaha na upendo. Na kwamba sote tunapaswa kulisha tumaini la watu hawa.