Papa Fransisko: Kuteseka na hali ngumu kwa uvumilivu na kushinda ugandamizwaji kwa
upendo.
Mkristu anapaswa kustahimili, kuvumilia mateso, na kushinda ukandamizwaji wa nje
na ndani, kwa upendo , ni msisitizo uliotolewa na Papa Fransisko wakati akiongoza
Ibada ya Misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta mapema asubuhi siku ya Ijumaa, ambayo
ilikuwa ni Siku Kuu ya Mama Maria, Msaada wa Wakristo.
Katika hotuba yake,
Papa Fransisko , aliomba neema mbili ambazo ni kustahimili kwa uvumilivu na kupata
ushindi kwa njia ya upendo. Alitaja hizi ni neema mbili halisi kwa Mkristu. Papa alionyesha
kutambua kwamba, uvumilivu katika mateso, si jambo jepesi katika hali zote iwe mateso
ya kiroho au kimwili au kutokana na matatizo mengine ya nje ya kijamii, bado ni mateso
yanayoumiza roho ya mtu. Lakini katika kuteseka Papa anasema si tu kama jambo jepesi
la kuyavumilia mateso, lakini ni wakati wa kuyabeba mateso kwa nguvu zaidi ili kwamba
matatizo hayo, yasituangushwe chini.
Ni kuendelea kuwa imara na tena kwa
ushupavu zaidi. Huo ndiyo uadilifu wa Kikristo. Papa alieleza na kumrejea Mtakatifu
Paulo, anaongea mara kadhaa juu ya kupokea na kuyavumilia mateso, kwa ushupavu zaidi,
kukataa kushindwa na matatizo. Na hili linapata maana kwamba, kwa Mkristo, mateso
ni kigezo cha kuiimarisha zaidi imani yake. Ingawa si jambo jepesi, na hasa kutokana
na vishawishi vya mambo mengine yanayolenga kudhoofisha imani, Mkristu anapaswa kuvikataa
vishawishi hivyo na kuyavumilia mateso kama silaha yake ya kumuirisha zaidi, kwa muono
kwamba, mateso ni neema kuvumilia. Na hivyo katika matatizo ni lazima kuiomba neema
hii . Papa aliiigeukia neema ya ushindi kwa upendo, akisema, kuna njia nyingi
za kupata ushindi lakini kwa neema ya upendo tunayoimba, nayo pia si rahisi, hasa
pale tunapokuwa na maadui nje wanao tupata mateso makubwa , inakuwa ni mtihani mgumu
kuupata ushindi kwa njia ya upendo. Mara nyingi kishawishi cha kutaka kulipiza kisasi
huonekana kwa nguvu zaidi, kama ndiyo jibu sahihi la kuzia mashambulizi dhidi ya adui.
Lakini Yesu alitufundisha kuwa wanyenyekevu na pole, kwamba upole ni ushindi, kama
Mtume Yohana anatuambia katika barua yake ya kwanza: Upendo ni ushindi wetu, na imani
yetu'. Imani yetu ni kwamba , Yesu, alitufundisha upendo na alitufundisha kumpenda
kila mtu. Na kwamba, sisi tunakuwa na upendo wakati tunapowaombea adui zetu, na
kuwapenda.
Ingawa kuwaombea maadui zetu wanaotufanya tuteseke pia si jambo
jepesi , lakini Mkristu hupata nguvu za kufanya hivyo kwa utambuzi kwamba , ushindi
wake unaweza kupotea, pale anaposhindwa kusamehe maadui na kama hawezi kuomba kwa
ajili yao. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa Wakristo wanaye shindwa kuomba neema hii ya
upendo, humezwa na huzuni na kukata tamaa, kwa sababu hana tena neema ya kustahilimili,
uvumilivu na ushindi kwa upendo":
Papa alikamilisha homilia yake akiomba
msaaada wa Mama Maria, Msaada wa Wakristu , ili Bwana awajalie wafuasi wake Neema
ya neema ya kustahimili , uvumilivu na kushinda kwa upendo. Na kwmaba kuna wengi
walioichukua njia hii nzuri , ambao hawana mengi ya kueleza ili miyo yao imejazwa
na upendo. Wnajua namna ya kumsamehe adui na wanajua jinsi ya kuwaombea Maadui . Na
hivyo ndivyo Wakristo wanayotakiwa kufanya.
Ibada hii ya Misa ilihudhuriwa
na wafanyakazi katika Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mawasiliano Jamii, akiwepo pia
Rasi wa Baraza hilo, Askofu Mkuu Claudio Maria Celli. Siku hiyo pia Mama Kanisa alikuwa
akitolea maombi yake kwa ajili ya Kanisa nchini China. Katibu Mkuu wa Shirika kwa
ajili ya Uinjilishaji wa Watu , na kikundi cha Mapadre , watawa na Waseminaristi na
walei kutoka China pia walihudhuria Ibada hiyo.