2013-05-24 10:50:15

Wapenda haki na amani wasikitishwa na vitendo vya vurugu nchini Tanzania!


Askofu mkuu Protase Rugambwa, Katibu mwambata na Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kazi za Kimissionari katika mahojiano maalum na Radio Vatican anasema, matukio ya uvunjifu wa misingi ya haki, amani, utulivu na mshikamano wa kitaifa nchini Tanzania ni changamoto na tatizo kubwa linalopaswa kushughulikiwa kwa umakini mkubwa. RealAudioMP3

Watanzania wote kila mtu kaadiri ya uwezo wake, wakae pamoja na kuanza mchakato utakaolisaidia taifa kurudi katika hali yake ya zamani, iliyoitambulisha kuwa ni kisiwa cha amani. Askofu mkuu Rugambwa anapenda kuchukua nafasi hii kutuma salam zake za rambi rambi kwa wote waliofikwa na majanga ya madhulumu ya kidini pamoja na ghasia zinazoendelea kufuka moshi. Anatoa pole pia kwa wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine. Anasema, amani ni jambo la msingi kwa ustawi na maendeleo ya watu.







All the contents on this site are copyrighted ©.