Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Tanzania Dk. Emmanuel Nchimbi alionya kuwa tabia
na inayoanza kujengeka ya kila eneo kutaka inufaike peke yake kutokana ralimalia ya
taifa iliyopo kwenye eneo husika italigawa taifa. Dk. Nchimbi amesema kuna baadhi
ya taasisi za kiraia na vyama vya siasa kutokana na maslahi binafsi yasiyo na upeo
mpana vinaweza kudhani kuunga mkono madai ya namna hiyo vinaweza kukubalika na jamii.
Alisema
watu kama hao wataipasua nchi na kusababisha vifo vya maelfu na majeruhi huku akimtaka
kila kiongozi na mwananchi atambue anayo dhamana ya kuendeleza haki, amani na kuchangia
maendeleo. Amesema wapo wasaliti wa taifa la Tanzania ambao wanajua maendeleo makubwa
yanayoweza kupatikana Mkoani Mtwara na Tanzania kwa ujumla kutokana na gesi hivyo,
wanatumia vibaya ufahamu wao mdogo kuhusu gesi na kuchochea upinzani dhidi ya mradi
huu unaotarajiwa kuwakomboa Wanamtwara na Watanzania kwa ujumla.
Akizungumzia
kuhusu vurugu hizo, Waziri Nchimbi amesema jumla ya watu 91 wamekamatwa kwa makosa
ya kufanya mikusanyiko isiyo halali na uharibifu wa miundombinu. Amesema hata hivyo
vurugu zimedhibitiwa huku polisi wakiendeleza oparesheni ya kuhakikisha hali ya usalama
inarejea huku akiwapongeza kwa kazi waliyofanya pamoja na uchache wao.
Katika
hatua nyingine alisema askari wanne kati ya 32 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
kutoka Nachingwe waliokuwa wakienda mjini humo kuongeza nguvu za kudhibiti vurugu
hizo walikufa baada ya gari la kupata ajali huku 20 wakijeruhiwa. Waziri wa Mambo
ya Nani ya Nchi amesema kuwa hadi sasa mtu mmoja aliyefahamika kama Karim Shaibu katika
vurugu hizo wakati Askari Polisi wawili walijeruhiwa kwa bomu la kishindo.
Akizungumzia
kuhusu uharibifu uliotokea amesema ofisi ya Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnain Murji
(CCM) iliyopo Mikindani imeharibiwa vibaya na kuharibiwa vitu vilivyokuwemo wakati
nyumba za askari wanne zimevunjwa na kubwa vitu mbalimbali.
Ameongeza kuwa
ofisi ya Mahakama ya Mwanzo, ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chikongola,
nyumba ya mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Kassimu Mikongoro
zimechomwa moto. Pia nyumba ya ofisa Mtendaji Kata ya Magomeni imechomwa moto lakini
Nchimbi amesema bado thamani halisi ya mali zote zilizoungua na kuharibiwa bado haijapatikana.