Ripoti ya mwaka ya Mamlaka ya Usimamizi wa fedha za Vatican
Jumatano, Ofisi ya habari ya Vatican, ilikuwa mwenyeji wa Mkutano kwa ajili ya uzinduzi
wa Ripoti ya Mwaka 2012 ya Mamlaka ya Fedha (AIF). Mkurugenzi wa Mamlaka hayo ,
Rene Brülhart, alitaja ushirikiano wa ofisi mbalimbali za Vatican katika kukabiliana
na matumizi mabaya ya mfumo wa fedha wa Vatican. AIF ni mamlaka husika ya Jimbo
Takatifu na Nchi ya Vatican, kwa ajili ya usimamizi na udhibiti wa fedha zinazopita
ktatika mfumo wa fedha wa Vatican, zisitumike kufadhili ugaidi. AIF ilianzishwa
mwaka 2010 na kuanza kazi zake rasmi Aprili ya 2011. Hii ni mara ya kwanza kwa
Ofisi ya Habari ya Fedha katika mamlaka ya AIF, ya Jimbo Takatifu na nchi ya Vatican
kuchapisha na kuwasilishwa taarifa yake ya mwaka hadharani. Ripoti hiyo ni mapitio
juu ya shughuli na takwimu za AIF, kwa mwaka mzima 2012. Ripoti inabaini, katika
kipindi hiki cha mwaka 2012 ,AIF, kumetolewa tuhuma sita, katika huduma za kuhamisha
na kuingiza fedha katika mfumo wa fedha wa Vatican ambapo mwaka juzi, ilikuwa ni
kesi moja tu iliyotolewa. Kati ya kesi hizo sita, mbili ziliwasilishwa katika Kitengo
cha sheria cha Vatican kwa uchunguzi zaidi. Na kwamba takwimu na mwelekeo tangu
mwanzo wa 2012 unatia moyo na kuonyesha kwamba , mfumo wa fedha unaendelea kuboreshwa.
Rene Brülhart, Mkurugenzi wa AIF, aliendelea kuuambia mkutano kwamba, mwaka 2012,
AIF pia ilianzisha mfumo wa kuchunguza utaratibu katika uchambuzi wa uhamishaji wa
Fedha kwa mujibu wa vyombo vya kisheria, katika kukabiliana kikamilifu na matumizi
mabaya ya uwezo wa mfumo wa fedha wa Jimbo Takatifu na Vatican. Juhudi hizi walizifanya
kwa kushirikiana kwa ukaribu zaidi na Sekretarieti ya Nchi, Mfumo wa Ulinzi wa Vatican
(Gendarmeria), na watetezi wa Sheria na taasisi chini ya usimamizi wa AIF, ili kuboresha
ufahamu na usalama, na kuhakikisha uratibu wa ndani ya ushirikiano katika masuala
yote ya uingizaji na hamishaji wa fedha kutoka taasisi za fedha za Vatican. Na
zaidi kipengele muhimu katika ripoti hiyo ni mafanikio yaliyopatikana katika ushirikiano
wa kimataifa, unaoonyesha wazi uwajibikaji wa Jimbo la Papa katika kuw Mbia aminifu
kimataifa, katika lengo la kukabiliana na uwepo wa fedha chafu. Mwaka 2012, kulitiwa
saini hati ya Mkataba wa Makubaliano na Mamlaka husika, nchini Ubelgiji na Hispania.
Mkataba huo, unaendelea kuwa sera ya utendaji kwa mwaka 2013, ili kuendeleza uimarishaji
wa ushirikiano wa kimataifa, katika utiaji wa sahihi katika mikataba kadhaa ya Makubaliano,
ushirikiano na Ubia na nchi nyingine husika na mamlaka. Katika Ripoti hii ya
mwaka 2012, Mkurugenzi Rene Brülhart, anasema mtazamo kwa ajili ya 2013 inaendelea
kukaza uimarishaji zaidi wa mfumo wa fedha zinazoingia na kutoka AML / CFT, ikiwa
ni pamoja na utekelezaji wa Mapendekezo Moneyval kupitia sheria mpya zinazofaa au
kufanyiwa marekebisho na mwendelezo wa ufahamu, kwa ajili ya kuimarisha mchakato fedha
katika mamlaka zote husika na taasisi.