2013-05-23 14:30:04

Papa Francisko kutembelea mji wa Assisi hapo tarehe 4 Oktoba 2013


Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi lililotolewa na Askofu Domenico Sorrentino wa Jimbo la Assisi-Nocera Umbra-Guardo Tadino, nchini Italia la kutembelea Assisi hapo tarehe 4 Oktoba 2013. Baba Mtakatifu Francisko anasema kwamba, Mji wa Assisi una umaarufu wake. Anawatakia maandalizi mema kwa ajili ya hija hii ya kichungaji na anawaomba ili waendelee kumwombea katika maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.







All the contents on this site are copyrighted ©.