Ijumaa , tuwakumbuke Wakristu wa China katika sala- wito wa Papa
Papa Fransisko ametoa ombi kwa Wakristo duniani kote, Ijumaa ya wiki hii, kutolea
sala kwa ajili ya Wakristu nchini China. Akizungumza mwishoni mwa Katekesi yake
kwa mahujaji na wageni waliofika kumsikiliza katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu
Petro siku ya Jumatano, Baba Mtakatifu aliutumia muda huo, kutoa ombi lake la kuwataka
wakristu duniani kote Ijumaa, Mei 24 2013, waungane katika sala kuwaombea Wakristu
wa China. Tarehe hii 24 Me1, iliwekwa wakfu kwa ajili ya kumbukumbu ya kiliturujia
ya Bikira Maria, Msaada wa Wakristo, anayeheshimiwa kwa msisimko mkubwa wa ibada katika
Madhabahu ya Sheshani Shanghai, kuwa siku ya kuuungana kiroho kwa ajili ya kuwaombea
Wakristu wote wa China. Alisema, "Naomba Wakatoliki wote duniani kujiunga katika
sala pamoja na ndugu na dada zetu wa China, kuomba kwa Mungu, neema ya kutangaza
kwa unyenyekevu furaha ya Kristu, aliyekufa na kufufuka, na pia katika kuwa aminifu
kwa Kanisa lake na Khalifa wa Mtume Petro, na kuyaishi maisha ya kila siku katika
huduma ya taifa lao na kwa wananchi wenzao, kwa njia ambayo ni thabiti katika imani
wanayo ikiri.
Papa alitoa ombi lake huku akiongeza kwamba , kwa maneno yetu
wenyewe machache ya sala, kwa Mama wa Sheshani, pamoja nanyi, alipenda kutolea
sala kwa Mama Bikira Maria: "Mama yetu wa Sheshani, awadumishe waamini wote wa Kanisa
nchini China, ambao,licha ya kukabiliwa na majaribumakali kila siku , bado wanaendelea
kuamini, kwa matumaini na upendo. Kamwe na wasipatwe na woga na hofu ya kumtangaza
Yesu ulimwenguni , na dunia kote.
Papa alisali ili Mama Maria, Bikira mwaminifu,
, msaada Wakatoliki Kichina, awe msaada wa kutimiza wajibu wao , licha kwamba si rahisi,
lakini wa thamani sana katika macho ya Bwana, katika kuulisha mapenzi na ushiriki
wa Kanisa nchini China, kwenye umoja wa hija nzima ya kanisa la Ulimwengu. .
Pia
ilikumbusha Mei 2008, Papa-mstaafu, Benedict XVI, alitoa wito kwamba, katika adhimisho
la Siku Kuu ya Mama yetu, Msaada wa Wakristo , Siku inayoheshimiwa sana katika Madhabahu
ya Sheshani, karibu na Shanghai Mei 24 ya kila mwaka, iwe ni Siku ya Dunia ya kutolea
sala maalum kwa ajili ya taifa la China.