Baba Mtakatifu Francis, Jumanne mara baada ya kupata taarifa za kimbunga kikali kilichopita
katika mji wa Oklahama Marekani, alipeleka salaam zake za rambirambi kwa waathirika
wote na uongozi mahalia kupitia Mjumbe wake Askofu Mkuu Paulo Coakley, Askofu Mkuu
wa jiji la Oklahoma. Katika ujumbe huo, Papa ametaja mshikamano wake wa karibu
na wote, kupitia njia ya sala na maombi kwa Bwana mwenye huruma na tumaini la maisha.
Na ameonyesha kujali hasara ya kutisha ya maisha yaliyokatizwa na pia kazi kubwa
inayowakabili sasa, ya kuujenga upya mji huo na vitongoji vyake. Na amewaombea
wote walio fariki katika janga hili, mapumziko katika amani ya Bwana wa milele,
nao wafiwa na walio katika mateso wapate kuwa na faraja za Kristu Mfufuka, licha ya
mateso wanayopata sasa, na hasa kwa kukosa makazi au majeruhi. Kwa namna ya pekee,
ametolea sala kwa Mungu mwenye huruma nyingi awafariji hasa vijana na watoto katika
wakati huu mgumu wa maombolezo na familia zao. Pia amewaombea viongozi mahalia
na viongozi wa kidini na kwao wote wanaohusika na jitihada za kutoa misaada, wapate
zawadi ya Kristu, Bwana wa uweza , nguvu, faraja, na uvumilivu na matumaini mapya
mema.
Baba Mtakatifu Francis, Jumanne mara baada ya kupata taarifa
za kimbunga kikali kilichopita katika mji wa Oklahama Marekani, alipeleka salaam zake
za rambirambi kwa waathirika wote na uongozi mahalia kupitia Mjumbe wake Askofu Mkuu
PAULO S. Coakley, Askofu Mkuu wa jiji la Oklahoma. Katika ujumbe huo, Papa ametaja
mshikamano na ukaribu wake kwa wote kupitianjia ya sala namaombi kwa Bwana mwenye
huruma na tumaini la maisha. Na ameonyesha kujali hasara ya kutisha ya maisha yaliyokatizwa
na pia kazi kubwa inayowakabili sasa, ya kuujenga upya mji huo na vitongoji vyake.
Na amewaombea wote walio fariki katika janga hili, mapumziko katika amani ya bwana
wa milele, nao wafiwa na walio katika mateso wapate kuwa na faraja za Kristu Mfufuka,
licha ya mateso wanayopata sasa, na hasa kwa kukosa makazi au majeruhi. Kwa
namna ya pekee, ametolea sala kwa Mungu mwenye huruma nyingi awafariji hasa vijana
na watoto katika wakati huu mgumu wa maombolezo na familia zao. Pia amewaombea
viongozi mahalia na viongozi wa kidini na kwao wote wanaohusika na jitihada za kutoa
misaada, wapate zawadi ya Kristu, Bwana wa uweza , nguvu, faraja, na uvumilivu
na matumaini mapya mema.