Jumanne pia Baba Mtakatifu Fransisko, alitembelea nyumba inayotoa msaada wa kihali
kwa maskini inayoitwa "Casa Dono di Maria, inayoendeshwa na Shirika la Upendo la Mama
Tereza wa Calcutta. Papa Fransisko alifanya ziara katika nyumba hii, ililyoko
katika kuta za Vatican, kwa nia ya kushiriki adhimisho la miaka 25, tangu kufunguliwa
kwake. Katika hotuba yake , Papa aliiwashukuru kwa dhati, watawa wanaohudumia
nyumba hiyo, kwa kujali idadi kubwa ya watu wahitaji, wanaowalisha na kuwanyweshana
kutibiwa majeraha na hasa majeraha ya kiroho. Papa aliitaja miaka hii 25 kwamba yote
imekuwa ni miaka ya msamaria mwema , anaye mwinamia mhitaji na kumpa msaada , na ndivyo
wao pia wanavyokuwa wasamaria wema. Nyumba hii , iliyoko ndani ya jiji la Vatican
karibu na jengo la Ofisi ya Shirika kwa ajili ya Imani Sadikifu, hulisha wastani wa
watu maskini 60 kila siku na hutoa nafasi ya malazi kwa wanawake 25. Jengo hili lilizinduliwa
na Mwenye Heri Yohane Paulo 11 , kama matokeo ya Mwenye Heri Yohane Paulo 11 kukutana
na Mwenyeheri Tereza wa Calcutta. Papa Fransisko akiwa mahali hapo , alisema
jengo hili linapaswa kukumbusha jumuiya ya Wakristu , na kwa jiji lote na wakazi wote
wa Roma, kujenga familia thabiti kwa ajili ya kwuapokea wahitaji, ni kuwa na nyumba
iliyo tayari kupokea wageni na kuhudumia na kujenga udugu zaidi. Pia Papa alizumgumzia
umuhimu wa mtu kujitolea sadaka kwa uhuru kamili na kuwa tayari kuhudumia mwingine,
majitoleo ya kama zawadi kwa wengine, kuwa zawadi huru ya ukarimu na mshikamano.
Papa kwa uyenyekevu, aliwapa Baraka zake za Kitume akiwamobea ili Mwenyezi Mungu ,
awape nguvu za kuendelea na utume huo, ishara wazi ya huruma ya Yesu katika dunia
ya leo.