2013-05-21 15:23:55

Umoja wa Wakristu ni muhimu hata katiak ushirikiano wa kibara


Mchakato wa Wakristu kuungana kiekumene ni muhimu kuchukuliwa kuwa ni mchango mkubwa katika kudumisha hali halisi za baadaye za siasa ya ubinadamu hasa katika dunia ya Magharibi. Na hivyo ushindi mpya wa umoja wa makanisa ya Kikristo, unakuwa ni msukumo mpya katika utendaji wa pamoja wa muungano wa Ulaya hasa katika kupambana na changamoto zilizpo kama mgogoro wa uchumi.
Haya ni maoni ya Kadrinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Kukuza Umoja wa Kikristo, alipo zungumza Ijumaa iliyopita, wakati wa kukamilisha Mjadala juu ya Pentecoste katika mtazamo wa ushirikiano kati ya Ulaya na Marekani, majadiliano yaliyofanyika katika Kanisa Schloss Seggau, Austria.
Alisema, katika hali halisi msingi za matatizo ya kiroho barani Ulaya, miongoni mwa mambo mengine, ni ukana Mungu na ubinafishaji utendaji wa kidini, ambavyo leo hii vinavyonekana kutaka kuwa tabia ya Ulaya na hivyo kuleta mshuko wa maendeleo katika ubinadamu, na matokeo yake yasionekana waziwazi lakini yanatisha, kama ilivyokuwa katika nchi za Magharibi katika karne ya kumi na sita ambamo kulifanyika vita vya umwagaji damu kwa ajili ya kuttea dini.
Kardinali alieleza na kuelekeza mawazo katika mapambano kati ya Wakatoliki na Waprotestanti,ya karne ya kumi na sita , akisema zaidi ya yote , ilikuwa ni ubinafsi wa kimadhehebu,uliosukuma nje umoja wa Wakristu na amani kijamii. Kardinali Kurt , anaendelea kueleza kwamba Makanisa haya yote yalifanya makosa makubwa katika muono wa kidini na jamii kwa ujumla. Alieleza na kurejea maelezo ya mwana teolojia Makatoliki wa Ujeruman, Johann Baptist Metz,aliyesema, machafuko na utengano huo, ulibinafisisha Ukristo, na kuingiza dini nyenyewe katiak utengano na machafuko na hivyo ilikuwa ni kuubinya uhuru wa uogofu na utendaji wa Mkristu katika maisha ya kijamii.

Kwa mujibu wa Kardinali Kurt, Rais wa Baraza la Kipapa, harakati za kiekumeni, Vikundi vya Kiekumene , vinatakiwa kutenda kinyume na kila changamoto inayotaka kudhoofisha umoja a Wakristu aliyotamani Yesu mwenyewe. Pia Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatikani, inaona haja ya kurejesha umoja wa Wakristo kama moja ya kazi yake kuu. Lakini hili linawezekana tu iwapo Makanisa yataweza kufanya toba kusameheana na kuridhiana, na kufanya kazi katika hali ya kuaminika kwa ajili ya uendelezaji wa marekebisho kwa ajili ya ujenzi mpya wa umoja na amani hata kijamii.

Na hii inapaswa kufanywa kupitia maisha ya kushirikishana kwa ajili ya umoja wa watu", kama ilivyo tajwa katika Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, katika ulimwengu huu wa watu waliojaw ana roho ya kusambaratika, w chuki na utafutaji wa maslahi ya kutatanisha kw amanufaa binafisi.
Wakati wa kuhitimisha Mkutano, Kardinali Kurt, alizungumzia uwiano kati ya Ulaya na ekumeni. Na washiriki wote walionekana kupendelea Uekumene kama neema ya barala Ulaya. Lakini Kardinali aliasa juu ya ukosefu wa utambuzi, katika utendaji kwamba, neema si rahisi kuwepo iwapo maisha ya kijamii hayashuhudii umoja na mshikamano wa kiekumene.

Ni kweli kuna mawazo mengi juu ya umoja ndani ya Makanisa. Lakini, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Kukuza Umoja wa Kikristo aliongeza , sera ya Ulaya ni lazima kuwa zaidi ya katoliki kwa maana ya kuwa na mabadiliko ya wote, na kushukuru kwa ukweli kwamba Papa Francesco, ametoka Amerika ya Kusini , na hivyo hii inazidi kudhihirisha kwamba Kanisa si la Ulaya peke yake, lakini kitovu cha dunia kwa ajili ya Wakaristu wote iwe Amerika ya Kusini, Afrika, Asia Marekani n.k.








All the contents on this site are copyrighted ©.