2013-05-20 14:57:26

Malkia wa Mbingu : zawadi na hazina ya Kanisa..Papa


Jumapili kabla ya kuongoza sala ya Malkia wa Mbingu, Baba Mtakatifu Fransisko, aliwaambia waamini waliokuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, na mitaa yake kwamba , wao pia ni zawadi na hazina ya kanisa.
Uwanja wa Mtakatifu Petro ulifurishwa na watu wapatao 200,000, kundi kubwa, wakiwa ni vikundi vipya vya kitume na jumuiya za Kikanisa vya walei, ambao tangu Jumamosi walimiminika mjini Roma toka pande mbalimbali za dunia kwa ajili ya kushiriki katika Ibada ya Mkesha wa Pentekoste kama Papa Francisko, alivyoomba kusali pamoja na vikundi na jumuiya hizo wakati wa Siku Kuu ya Kushuka kwa Roho Mtakatifu, kama sehemu ya maadhimisho ya mwaka wa Imani.
Siku Kuu ya hii ni kumbukumbu ya kushuka kwa Roho Mtakatifu, ambayo huadhimishwa kila mwaka kama ishara ya kufunga maadhimisho ya Kipindi cha Pasaka, na pia ni maadhimisho ya kumbukumbu ya maneno ya Yesu mwenyewe, kwa wafuasi wake, mimi na kwenda kwa baba lakini hamtakuwa peke bali nitamtuma Roho Mtakatifu kuwa nanyi.
Papa alisema, kama ilivyokuwa kwa mitume wake wakiwa wamekusanyika katika Chumba cha Juu kusali wakiwa na Mama Maria, Jumapili, ndivyo Roho Mtakatifu alivyoubadili uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kuwa kama chumba cha wazi cha juu, waamini kuuishi uzoefu wa kipindi cha mwanzo wa Kanisa, wakiwa wamekusanyika kama watu wa vipaji mbalimbali, wakifurahia uzuri huu wa kuwa wamoja. Papa alisema hiyo ni kazi ya Roho Mtakatifu, ambaye daima hutengeneza umoja mpya katika kanisa .
Baba Mtakatifu alivishukuru vyama, vikundi na jumuiya zote za Kikanisa, akisema nyinyi ni zawadi na hazina ya kanisa . Na kwa namna ya pekee aliwashikuru wote kwa kuja Roma kutoka pande mbalimbali za dunia. Na kwamba daima wamefanikishwa kwa uweza wa Injili ya Bwana. Na aliwataka wasiogope , daima wafurahi na kuwa pia wavumilivu, kwa ajili ya umoja wa Kanisa la Kristu Mfufuka aliye pamoja nao daima na pia aliwaweka chini ya ulinzi wa Mama Bikira Maria.

Papa pia alikumbuka kutolea sala zake kwa ajili ya maafa ya mafuriko na maporomoko ya aridhi yaliyotokea huko Emilia Romagna Italia na pia alitolea sala kwa ajili ya Shirikisho la watu wa kujitolea wa Italia “ONCOLOGY “.
Baada ya hotuba yake Papa akiwa ndani ya gari la wazi aliwazungukia waamini akiwasalimia, kuwashukuru na kuwabariki.

Na wakati wa kukamilika kwa Ibada ya mIsa kwa ajili ya Siku Kuu ya Pentecoste, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Ukuzajiwa Uinjlishaji Mpya, Askofu Mkuu Rino Fisichella, kwa niaba ya vyama vya walei na jumuiya za kikanisa, alitoa shukurani za dhati kwa Papa Fransisko, kwa homilia yake ya kusisimua na kuwatia nguvu mpya , za kusonga mbele na utume wao kwa ajili ya Kanisa.








All the contents on this site are copyrighted ©.