Imani katika sala, unyenyekevu, na moyo wa ushujaa hutenda miujiza
Sala ujasiri nyenyekevu na uthabiti, hufanikisha miujiza: Papa alieleza hili, mapema
Jumatatu wakati akiongoza Ibada ya Misa, katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta la
mjini Vatican. Ibada iliyohudhuriwa na baadhi ya wafanyakazi wa Radio Vatican, wakiwa
wameandamana na Mkurugenzi wao Padre Federico Lombardi. Homilia ya Papa kwa wafanyakazi
hao, ilirejea Liturujia ya Neno la siku, kifungu cha Injili ambamo wafuasi wa Yesu
walishindwa kumponya kijana mdogo mgonjwa, na Yesu aliwajibu kwamba wameshindwa kumponya
kijana huyo kwa sababu wana imani haba. Baba wa Kijana huyo kwa imani thabiti, aliomba
msaada kwa Yesu. Na Yesu anawaambia kila kitu kinawezekana kwa anayeamini. Papa
Francesco alieleza, mara nyingi wapo wanaopenda kuwa wafuasi wa Yesu, lakini hawapendi
kuhatarisha mengine wanaoyoyaamini na hivyo imani yao kwa Kristu inakuwa ni imani
nusunusu, hawana imani nae kikamilifu. Papa alieleza na kuhoji kwa nini hali hi ya
kutosadiki kikamilifui? Na alitoa jibu kwamba, wao wana amini kwamba, ni moyo wenyewe
usiotaka kujifunua wazi, moyo unabaki umefungwa , lakini katika ukweli wake moyo
huo unaotamani kuwa na imani thabiti.
Hivyo basi, binadamu anaushinikiza
moyo kutojifunua na wala kujiweka chini ya maongozi ya Yesu, kama ilivyokuwa wakati
ule, wanafunzi wa Yesu walimwuliza kwa nini, hawakuweza kumponya kijana, na Bwana
aliwajibu kwamba aina mapepo yaliyomshambulia kijana huyo, hayawezi kutolewa nje
na jambo lolote , isipokuwa kwa sala tu. Papa alieleza na kusema, ingawa tunamtolea
sala Bwana,ndani mwetu tuna kigugumizi cha imani. Hatuna imani thabiti na yule tunayemtolea
maombi yetu lakini twayatolea maombi hayo kama majaribio au mazoea ya kusali. Ili
Bwana aweze kuyaitikia maombi yetu, twapaswa kusadiki kwamba kile tunachomwomba Bwana
atakifanikisha. Na hii ni kuwa na imani thabiti katika nguvu ya sala, ni kusadiki
kw unyenyekevu kwamba, Yesu ni nguvu na anaweza kufanya muujiza. Kuomba muujiza
wa uponyaji , au kuomba mabadiliko katika mahusiano ni lazima kuambatane na sala
thabiti inayotuhusisha sisi sote. Papa Francisko alieeleza na kutolea mfano wa tukio
hilo lilitokea huko Argentina, ambako : mtoto wa miaka 7 aliugua na madaktari kutoa
masaa machache ya maisha. Baba yake, fundi umeme, mtu wa imani, akiwa kama amepagawa
na habari hii ya maisha ya mtoto wake kufika ukingoni, alipanda basi na kwenda katiak
madhabahu ya Mama Bikira Maria ya Lulijan, umbali wa 70 km mbali, ambako alisali
na kumlilia Mungu ayaokoe maisha ya mwanae na Mungu alisikia sala yake na aliporejea
nyumbani alimkuta mtoto wake akiwa amepona. :
Papa alihitimisha homilia yake
akisema tunahitaji kuomba kwa moyo wa imani na ushujaa zaidi kwamba Mungu anaweza
kila jambo. Hakuna anayeweza kusema ni peke yake ni jasiri wa maombi, bali kila mmoja
ni jasiri, kinachotakiwa ni kuwa na Imani kwa Bwana. Papa alieleza na kuwataka wote
watoleee sala zao kwa imani thabiti kwa ajili ya watu wengi ambao wanakabiliwa katika
vita, wakimbizi wote na wote wnaokabiliwa na hali ngumu za maisha zilizo nje ya uwezo
wao akisemam twapaswa kusema, Bwana, naamini na msaada wangu utatoka kwako leo hii.
.