Rais Napolitano wa Italia kukutana na kuzungumza na Papa Francisko, hapo tarehe 8
Juni 2013
Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kukutana na kuzungumza na Rais wa Italia Giorgio
Napolitano hapo tarehe 8 Juni 2013. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Baba Mtakatifu
Francisko na Rais Giorgio Napolitano kukutana rasmi. Itakumbukwa kwamba, Rais Napolitano
alikuwa ni kati ya viongozi wakuu wa Serikali na Mashirika ya Kimataifa waliofika
mjini Vatican kushuhudia Baba Mtakatifu Francisko akianza utume wake kama Khalifa
wa Mtakatifu Petro.
Kama viongozi wengine alipata nafasi ya kusalimiana na
Baba Mtakatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro baada ya Maadhimisho ya Misa Takatifu.
Hayo yamebaionishwa na Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa Vatican.