2013-05-17 15:41:38

Padre Adolfo Nicolàs, SJ, achaguliwa kuwa ni Rais wa Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume Duniani


Askofu mkuu mteule Josè Rodriguez Carballo, Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume ametuma salam za pongezi kwa Mheshimiwa Padre Adolfo Nicolàs, S.J. Mkuu wa Shirika la Wayesuit kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Shirikisho la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume Duniani.

Kabla ya uteuzi huu, Padre Nicolàs alikuwa ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume. Nafasi hii inatarajiwa kujazwa wakati wa mkutano mkuu utakaofanyika mwezi Novemba 2013.







All the contents on this site are copyrighted ©.