Baba Mtakatifu Francisko wakati akitoa Katekesi yake kwa mahujaji na wageni waliokuwa
wamemiminika kwa wingi kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican,
jumatano iliyopita ameonesha nia ya kutaka kutembelea Madhabahu ya Bikira Maria wa
Bonaria yaliyoko Kisiwani Sardenia, mjini Cagliari nchini Italia na kwamba, kama hakutakuwepo
na kizuizi chochote basi, hija hii ya maisha ya kiroho angependa kuifanya Mwezi Septemba
2013. Hii ni kutokana na uhusiano wa kidugu na wa muda mrefu uliopo baina ya miji
ya Buenos Aires na Cagliari.
Mji wa Bueonos Aires ulipoanzishwa ulijulikana
kama mji wa Fumbo la Utatu Mtakatifu, lakini Mabaharia walipofika mjini hapo wakabadili
jina na kuita mji wa "Madonna wa Bonaria". Jina linalotumika hadi leo hii.