2013-05-16 15:40:07

Mabalozi wapya mjini Vatican wawasilisha hati zao za utambulisho!


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 16 Mei 2013 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wa Kyrgstan, Antigua, Barbuda, Lussenburg na Bostwana, watakaoziwakilisha nchi zao hapa mjini Vatican.

Balozi Lameck Nthekela alizaliwa tarehe 2 Novemba 1965. Baada ya masomo yake nchini Botswana alijipatia shahada ya kwanza katika masomo ya sayansi jamii kunako mwaka 1991. Akajiendeleza zaidi nchini Australia na kujipatia shahada ya uzamili kunako mwaka 1996.

Tangu wakati huo amefanya shughuli mbali mbali nchini Botswana. Alikwisha wahi kuajiriwa kwenye Taasisi ya taifa ya Afya, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na kuwa ni Meneja wa Maendeleo ya Biashara na uwekezaji kutoka nje, (BEDIA).

Kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2007 alikuwa ni Mwakilishi wa BEDIA huko London, Uingereza. Tangu wakati huo akateuliwa kuwa ni Meneja wa utafiti, kazi ambayo aliifanya kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2009. Kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2010 aliteuliwa kuwa Meneja wa Biashara ya Nje; Mwaka 2010 hadi mwaka 2011 akateuliwa kuwa Meneja wa huduma kwa ajili ya BEDIA na hatimaye, kuanzia mwaka 2011 hadi mwaka 2012 akateuliwa kuwa Mkurugenzi mtendaji wa BEDIA.







All the contents on this site are copyrighted ©.