2013-05-16 09:43:43

Katibu mkuu wa Chama cha Wakristo Nigeria auwawa kinyama!


Mchungaji Faye Pama Musa, aliyekuwa ni Katibu mkuu wa Umoja wa Wakristo nchini Nigeria ameuwawa kikatiliki nyumbani kwake siku ya Jumanne tarehe 14 Mei 2013 na watu wanaosadikiwa kuwa ni kutoka katika Kikundi cha Boko Haram kinachoendelea kutishia amani na usalama wa wananchi wa Nigeria.

Tukio hili limekuja muda mfupi tu baada ya Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria kutangaza hali ya hatari jambo ambalo limepelekea mashambulizi kadhaa katika maeneo ya Borno, Yobe na Adamwa. Chama cha Wakristo nchini Nigeria kimelipokea tukio hili kwa majonzi makubwa.







All the contents on this site are copyrighted ©.