Askofu mkuu Norbert Wendelin Mtega wa Jimbo kuu la Songea ang'atuka kutoka Madarakani!
Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi lililotolewa na Askofu mkuu Norbert Wendelin
Mtega wa Jimbo kuu la Songea, Tanzania kung'atuka kutoka madarakani kadiri ya sheria
za Kanisa Namba 401 kipengele namba 2.
Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua
Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wa Jimbo la Iringa na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki
Tanzania kuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo kuu la Songea hadi pale atakapoteuliwa
tena Askofu mkuu kushika nafasi hiyo.