Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM, kuanzia tarehe
2 Mei 2013 limeanzisha Shirika la Habari la SECAM na kumteua Don Bosco Ochieng Onyalla
kutoka Jimbo Katoliki la Rumbek, Sudan ya Kusini kuwa mkurugenzi wake wa kwanza. Makao
makuu ya Shirika hili litakalojulikana kama Catholic News Agency fo Africa, CANAA
yatakuwa Jijini Nairobi, Kenya.
Padre Onyalla amepewa dhamana ya kuanzisha
ofisi za habari kwa kushirikiana na Askofu mkuu Chrles G. Palmer Buckle wa Jimbo kuu
la Accra, Ghana ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Bodi ya CANAA. Padre Onyalla atakuwa
na wajibu wa kuhakikisha kwamba, anawasiliana na wadau mbali mbali wa habari kutoka
ndani na nje ya Bara la Afrika, ili kuunga mkono jitihada za kukuza na kuendeleza
mawasiliano ya jamii kama sehemu ya mchakato wa Uinjilishaji Mpya na ule wa kina.
Padre Onyalla alikuwa ni mwanzilishi wa Radio Good News ya Jimbo Katoliki
Rumbek hadi mwezi Oktoba 2012.