Ripoti ya nne juu ya hali ya uhai wa Mafundisho Jamii ya Kanisa imewasilishwa.
Alhamis , katika Makao Makuu ya Mafundisho Jamii ya Kanisa Ulimwenguni, kuliwasilishwa
"Ripoti ya Nne juu ya hali ya Uhai wa Mafundisho Jamii ya Kanisa ulimwengu". Ripoti
hiyo imetolewa na Mtazamji wa Kimataifa Shirika la Van Thuan , kwa kushirikiana na
Kikundi cha Kitume cha Kikristu (MCL). Na wametazama zaidi, hoja nzito za kimaadili
zisizokuwa na mbadala: maisha, familia, uhuru, amani na haki ya kijamii. Na Miongoni
mwa hoja za kidharura zinazo nyambuliwa zaidi kwa mwaka huu ni ukolonishaji wa asili
ya binadamu, matokeo yake katika upanuzi wa maendeleo ya kile kinachojulikana “itikadi
jinsia.”
Askofu Giampaolo Crepaldi, Askofu Mkuu wa Trieste na Rais wa Van Thuan,
katika maelezo yake ya wakati wa kuiwasilisha ripoti hiyo amesema, kinachohitajika
zaidi katika hoja hii ya itikadi za kijenda, zilizoanzishwa kwa kasi kubwa barani
Ulaya na kuenea haraka katika mataifa mengine, ya Ulaya , nchi zingine kama vile
Argentina, ni kutokwenda kinyume na utu wa biandamu na mwelekeo wa maisha adilifu
na maisha ya familia.
Alitaja Mienendo inayo jaribu kuharibu tendo la ndoa,
na binadamu kuwekwa katika hatari ya kudharirisha utu wake, imekuwa ni changamoto
kwa Kanisa, kufufua thamani ya "sheria ya asili" kama kituo rejea katika utoaji wa
maoni na Uinjilishaji Mpya.
Askofu Mkuu Cleopaldi ameasa juu ya dhania kwamba,
hali hizi halisi, na taratibu hizi kitamaduni, kisiasa na kijamii, hudhoofisha imani.
Lakini yeye ana imani kwamba, imani hukomaa zaidi kwa kupambana na changamoto.
Na hivyo hali hiyo hulazimu imani kujenga taratibu ambazo matokeo yake ni kuyabatilisha
yale ya kibinadamu. Ni hivyo inakuwa dhahiri kwamba, jibu katika masuala haya
ya imani , linapaswa kuwa lile lenye wa kuiamusha imani , na hasa kanisa kuondokana
na kuhofia mapambano, badala yake, changamoto zinakuwa ni mwanya mzuri wa kuushuhudia
ukweli kwa kutoa majibu ya kuaminika, na kushawishi. Kwa maana hiyo, utume
uliofumbatwa katika Mafundisho Jamii ya Kanisa ni kutetea vyema nafasi kanisa katika
umma, hasa thamani ya maisha ya binadamu na viumbe na tunu za maisha zisizokuwa na
mbadala.