2013-05-11 09:12:02

Papa Fransisko ampokea Papa Tawadros II wa Alexandria.


Patriaki Tawadros II, wa Kanisa la Kikoptiki la Kiotodosi, Upatriaki wa Alexandria ambaye pia ni Mkuu wa Kanisa la Kikoptiki la Misri, yupo ziarani Roma.

Ijumaa pamoja na kukutana na kusali pamoja na Papa Fransisko Vatican, pia aliyatembelea makao makuu ya Baraza la Kipapa kwa ajili ya Kukuza Umoja wa Kikristo na idara nyingine ya Curia ya Roma. Na kufanya hija katika makaburi ya Mitume Petro na Paulo. Pia alikutana na waamini waotodosi Wakoptiki, katika makao yao makuu ya hapa Roma.

Ziara Papa Tawadros II, inatajwa kuwa ya kihistoria kutokana na kwamba, kimepita kipindi cha miaka 40, tangu Mkuu wa Kanisa la Kikoptiki la Kiotodosi kumtembelea Papa wa Roma. Ziara ya mwisho ilifanywa na Mtangulizi wa Papa Tawadros, Papa Shenouda III, ambaye alikutana na Papa Paulo VI, Vatican, Mei 1973, miaka arobaini iliyopita.
Na kwamba, ziara ya Papa Tawadros, ina umuhimu wa kipekee kwa Kanisa la Kikoptiki la Misri , ambalo hivi karibu, limeweka sahihi katika azimio muhimu, lililoanzisha mazungumzo ya kiekumeni kati ya Makanisa haya mawili. Patriaki Tawadros II, tangu achaguliwe kuliogoza Kanisa la Kiotodosi la Kikoputiki Misri, amekwa akihimiza ukomavu wa jamii ya Kikristo Misri. Na hivi karibuni kumeundwa Baraza la Makanisa ya Kikristo la Misri.

Kanisa la Kikoptiki la Ki-Orthodox Misri, lina waumini wapatao millioni kumi, ikiwa ni idadi kubwa katika Kanisa lote la Kikoptiki katika eneo la kanisa la Mashariki ya Kati, ambalo kwa nyakati hizi linaishi katika hali ngumu za kisiasa.

Ijumaa, hotuba ya Papa Tawadros II kwa Papa Fransisko,ilipendekeza kwamba kila mwaka tarehe 10 Mei, iwe ni Siku ya sherehe ya pamoja kwa jumuiya hizi mbili. Na pia alitoa mwako kwa Khalifa wa Mtume Petro kulitembelea Kanisa Mtakatifu Marko la Misri, lililoanzishwa na Mtakatifu Marko Mwinjilisti katikati ya karne ya kwanza ya Ukristu.

Na hotuba ya Papa kwa mgeni wake Papa Tawadros II na ujumbe alioandamana nao, ililitaja tukio hili kuwa ni wakati wa furaha kubwa, kukutana katika kaburi la Mtume Petro katika hali ya amani na udugu kama ilivyokuwa miaka 40 iliyopita wakati Papa Paulo VI alipokutana na Papa Shenouda II.

Na aliitaja ziara hii kuwa ni utendaji muhimu katika uimarishaji wa kiungo cha urafiki na udugu ambayo tayari upo kati ya Kiti cha Mtakatifu Petro na Kiti cha Mtakatifu Marko, urithi wa idadi isiyoweza kutajwa ya wafia dini, wanateolojia , mamonaki na waamini wote wa Kristu, ambao wamekuwa wakiishuhudia Injili, kizazi hadi kizazi , na mara nyingi katika hali tofauti tofauti na ngumu.
Na kwamba miaka 40 iliyopita, watangulizi wao waliweka azimio msingi pamoja la kutembea katika njia hii ya kiekumene ambalo lilizaa Tume kwa ajili ya Majadiliano ya kiteolojia kati ya makanisa haya mawili na matokeo yake mazuri , yameweza kuandaa mazingira mapana zaidi katika majadiliano kati ya Kania Katoliki na familia yote ya Kanisa la Kiotodosi la Masahariki , majadiliano yanayoendelea kutoa matunda mazuri hata leo. Na kwamba wanatambua kwamba njia ya kufikia umoja kamili bado ni ndefu , lakini hawawezi kukata tamaa bali watasonga mbele nayo.







All the contents on this site are copyrighted ©.