2013-05-10 09:51:17

Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wa Rais William Ruto wana kesi ya kujibu!


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetupilia mbali ombi lililokuwa limetolewa na Serikali ya Kenya kutaka Umoja wa Mataifa kufuta kesi inayomkabili Rais Uhuru Kenyatta na wenzake kuhusiana na machafuko ya kisiasa yaliyojitokeza nchini humo mara baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika kunako mwaka 2007 na kusababisha watu zaidi ya 1,200 kupoteza maisha yao na wengine wengi kukosa makazi kwa kuhofia usalama wa maisha na mali zao.

Wanadiplomasia waliojadili mwenendo wa ombi hili kutoka katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanasema, Baraza hilo halina mamlaka ya kusitisha kesi ambayo imekwishafunguliwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita. Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wa Rais William Ruto wanakana makosa haya na kwamba, kesi hii inatarajiwa kuendelea tena kuanzia mwezi Julai, 2013.







All the contents on this site are copyrighted ©.