Radio Waamini Kenya inaadhimisha Kumbu kumbu ya Miaka 10 tangu ilipoanzishwa
Askofu Martini Kivuva wa Jimbo Katoliki la Machakosi Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Tume ya Mawasiliano ya Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika Maadhimisho ya Kumbu kumbu ya Miaka 10 tangu Radio Waamini inayomilikiwa
na kuendeshwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya ilipozinduliwa. Kilele cha Maadhimisho
hayo ni hapo tarehe 12 Mei 2013 sanjari na Maadhimisho ya Siku ya Upashanaji Habari
Ulimwenguni kwa mwaka 2013.
Tamasha la Vyombo vya Habari nchini Kenya limeandaliwa
na wadau wa vyombo vya Mawasiliano ya Jamii ndani ya Kanisa Katoliki nchini Kenya.
Ndani ya viunga vya Radio Vatican tunaye Padre Joseph G. Healey, MM, anayefanya utume
wake nchini Kenya akizungumzia umuhimu wa mitandao ya Kijamii kama majukwaa mapya
ya Uinjilishaji Mpya.