Maendeleo ya kweli ya binadamu hayawezi kufanikishwa na ubinafsi... Ni maelezo
yaliyomo katika barua ya tatu ya Patriaki Moraglia kwa Makanisa ya Venezia kwa ajili
ya mwaka wa Imani. Amesema, muonekano wa mtu, ni kipimo cha maendeleo ya kweli ya
binadamu. Na hili ni msingi wa Mafundisho ya kijamii ya Kanisa, kama ilivyo ainishwa
na waanzilishi wa mafundisho hayo , Mababa wa Kanisa katika Hati yao inayo timiza
miaka 50 ya uwepo wake.
Patriaki Fransisko Moraglio , ametoa Waraka wa tatu
wa Kichungaji kwa Kaniia la Venice, kama mchango wake, katika yale yanayotakiwa kuzingatiwa
na Wakristu, wakati wa maadhimisho ya mwaka huu wa imani, katika tafakari za yale
yaliyopendekezwa mwezi Octoba mwaka jana, wakati wa kuzinduliwa kwa mwaka wa Imani,
juu ya Madambiu “Imani ya Kikristu katika mtazamo wa kuenea kwa malimwengu”.
Waraka
huo mpya, unasisitiza umuhimu wa kugundua na kujifunza mafundisho ya kijamii ya Kanisa,
ambayo yanatoa sura mpya juu ya ufunuo wa kimungu na hoja za kumweka mtu kuwa ndiye
kiini cha maendeleo katika juhudi zote za utendaji wa jamii.
Waraka wa Patriaki
Moraglia, umerudia kutaja na kusisitiza juu ya Kanuni msingi ya kwanza , katika utendaji
wote , kwamba ni utakatifu wa maisha ya mtu, hadhi ya ubinadamu wa mtu, kwamba, hadhi
ya utu wake ndiyo msingi wa utendaji wote mzuri wa kijamii , umoja na mshikamano
wote wa binadamu.
Na hivyo mtu hapaswi kumezwa na fikira za kudhani au kujiona
kama ni yeye binafsi anajitosheleza, lakini daima azingatie kwamba, ni mmoja lakini
katika muungano na wengine. Ni mtu mmoja lakini katika uhusiano na wengine , na hakuna
kinachoweza kutengua hilo.
Hivyo, hakuna maendeleo ya kweli ya binadamu,
kama maendeleo hayo yanafanywa katika misingi ya utamaduni wa ubinafsi. Jamii ya
binadamu inapaswa kuishi katika lengo la mtu kwa manufaa ya wengine. Na ndiyo njia
ya kutembea nayo katika tafakari za mwaka huu wa Imani