2013-05-08 08:37:35

Nyongeza ya mishahara ya Wabunge yawachefua wananchi wa Kenya


Kardinali John Njue, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya ameonya mwelekeo wa Wabunge wa Kenya kutaka kuongezewa mishahara kwamba, si wazo jema kwa wakati huu ambapo watu wengi wanaendelea kuathirika kutokana na myumbo wa uchumi kimataifa.

Nyongeza ya mishahara ya wabunge itakuwa na athari kubwa kwa uchumi wa nchi ya Kenya ambao bado unaendelea kusua sua. Kardinali Njue anasema kuna mambo ambayo kwa sasa yanapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza na wala si nyongeza ya mishahara ya Wabunge.

Watu wa kawaida wanapaswa kufikiriwa kwanza kabla ya kuanza mchakato wa nyongeza ya mishahara ya wabunge anasema Kardinali John Njue. Taarifa kutoka Kenya zinabainisha kwamba, Bunge la Kumi na Moja tangu lilipoanza kikao chake limejielekeza zaidi kutaka kuongezewa mishahara na kufutiwa kodi, mawazo ambayo yamewachefua wananchi wengi wa Kenya.







All the contents on this site are copyrighted ©.