2013-05-08 15:34:57

Ninyi ni warithi wa utamaduni wa Upendo kwa Kanisa .."The Swiss Guards".


Askofu Mkuu Becciu amekitaja kikosi cha ulinzi kwa Papa “The Swiss Guards”kuwa ni warithi wa utamaduni wa upendo kwa Kanisa

Jumanne mchana, ndani ya Vatican kulifanyika tukio la kuapishwa kwa Kikosi cha Ulinzi kwa Papa “The Swiss Guards”. Na kutokana na hali mbaya ya hewa nje , walinzi hao wapatao 35 walikusanyika katika ukumbi wa Paulo V1, badala ya kuwa nje katika uwanja wa Mtakatifu Damas kama ilivyo kawaida yao kwenye tukio kama hili.

Maaskori hao walifanya tamasha la kila askari alikula kiapo upya kwa kuinua mkono wake wa kulia na kufanya ishara ya Utatu Mtakatifu , na mkono wake wa kushoto ukiwa umeshika bendera. Kiapo hicho kilifanyika katika lugha tatu rasmi: kijerumani, kifaransa na kiitaliano. Wengine waliohudhuria hafla hiyo, ni pamoja na wanaohusika na mamlaka ya Vatican na kikosi kingine cha Maaskari kinachotoa ulinzi Vatican, akiwepo pia Rais wa Shirikisho Uswisi, Ueli Maurer, na Balozi wa Uswisi kwa Jimbo Takatifu, Balozi Paulo Widmer.

Askofu Angelo Becciu, Naibu Katibu wa Jimbo Takatifu, hivi karibuni akizungumzia kikosi hiki cha “The Swiss guards” aliwaita walinzi hao , kuwa ni Warithi maalum wa kiroho katika huduma ya ujasiri wa ulinzi wa Papa wa tangu zamani.
Msgr. Angelo Becciu, alieleza hilo katika barua yake aliyoitoa siku ya Jumatatu asubuhi, kwa ajili ya maadhimisho ya sadaka ya Walinzi 147 wa Uswisi ambao mwaka 1527 walipoteza maisha yao, wakimlinda Papa , wakati wa machafuko katika mji wa Roma.
Amewataja vijana hao wa Uswiss, kuwa ni warithi wa utamaduni mkubwa wa upendo kwa Kanisa na Jimbo Takatifu, na kuwataka waendeleee kutembea katika njia hiyo. Na aliwaalika walinzi wapya, kuendeleza uchaguzi huo wa hiari usiokatika tangu miaka ya kale. Na kwamba huu ni wito wa kipekee na uwajibikaji katika kumhudumia Baba Mtakatifu mwenyewe. Na kwa kiapo walichofunga, aliongeza, wamekubali kuchukua kazi ya maana sana ya Mkristo, kuishuhudia imani yao, katika uso wa watu wengi, hasa mahujaji na watalii wanaokuja Vatican kila siku.








All the contents on this site are copyrighted ©.