Mafundisho ya Papa Fransisko kwa mahujaji na wageni Jumatano hii yanasema, katika
kipindi hiki cha maadhimisho ya Pasaka, kipindi tunachokiishi kwa furaha, tukiongozwa
na Liturujia ya Kanisa,tunaiishi furaha kamili ya Roho Mtakatifu tuliyopewa na isiyokuwa
na kipimo na aliyesulibiwa na kufufuka Yesu Kristu (Yn3:34). Huu ni wakati wa neema
unaokamilika kwa Sikukuu ya Pentekoste, wakati Kanisa linauishi upya uzoefu wa kumiminwa
kwa mwanga kwa Roho juu ya Maria na Mitume wa Yesu , walipokusanyika katika maombi
kwenye chumba cha juu ghorofani.
Papa Fransisko amehoja ni nani Roho Mtakatifu?
na kutoa jibu kwa kuirejea sala ya Nasadiki, ambayo Mkristu huikiri imani yake akisema,
"Naamini katika Roho Mtakatifu, Bwana na mtoaji wa uzima".
Papa amefafanua.,
huu ni ukweli wa kwanza ambao kila Mkristu huuzingatia wakati wa kukiri Imani yake,
ni kwamba Roho Mtakatifu ni Bwana. Hii ina maana kwamba Yeye ni Mungu kweli kama
ilivyo Baba na Mwana, na kwamba sisi tunapomkiri Roho Mtakatifu tunamuunganishwa
moja kwa moja na Baba na Mwana. Roho Mtakatifu, ni kweli, nafsi ya tatu ya Utatu
Mtakatifu, Roho Mtakatifu ambaye ni zawadi kubwa ya Kristo Mfufuka, aliye mfunua
katika akili zetu na mioyo yetu kupitia imani kwa Yesu, kuwa ni Mwana aliyetumwa
kutoka kwa Baba, ambaye hutuongoza katika urafiki, na kutuunganisha katika ushirika
na Mungu
Papa aliendelea kuangalisha katika ukweli kwamba Roho Mtakatifu ni
chanzo kisichokuwa na mwisho cha maisha ya kimungu ndani wetu. Katika nyakati zote
na kwa kila mtu, mna hamu ya kutaka kuwa na maisha makamilifu mazuri, maisha ya haki
na wema, maisha ambayo si ya kutishiwa na kifo, lakini ambayo yamaweza kukomaa na
kukua katika ukamilifu wake. Papa ameendelea kumweleza mtu kama ni msafiri anayevuka
jangwa la maisha, ana kiu ya maji yaliyo hai, maji yanayo miminika na safi, yenye
uwezo wa kuzima hamu yake ya kina katika kuupata mwanga wa uzuri wa upendo, na amani.
Na kwamba sisi wote, huisikia hamu hii. Na Yesu yuko tayari kutupatia maji yaliyo
hai: ambaye ni Roho Mtakatifu, atokaye kwa Baba na Mwana, Roho anayemiminwa katika
mioyo yetu. Yesu anatuambia kwamba "Nimekuja ili wawe na uzima na kuwa ni uzima kamili"
(Yohana 10, 10).