2013-05-07 10:38:43

Umoja wa Kitume, Sala na Uchaji: Mama Yetu wa Quintiliolo


Jumapili iliyopita, Katika Maadhimisho ya mwaka wa Imani , Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro ulipambwa na maelfu ya wawakilishi kutoka Mashirika na vyama vya kitume na Uchaji , walioitolea Jumapili hiyo kuwa ni Siku Maalum katika maadhimisho ya mwaka wa Imani, kwa ajili ya maisha yao ya umoja wa kitume sala na Uchaji.

Tukio hili walilianza tarehe 3 Mei, chini ya Mada : tangu katika mitaa ya dunia, shuhuda za imani , vyama vya kitume sala na uchaji , katika hija kwenye kaburi la Mtakatifu Petro, kwa ajili ya Uinjilishaji mpya. Mahujaji hao walitembelea Kaburi la Mtakatifu Petro, mapema siku ya Jumamosi .
Mapema , Askofu Mkuu Rino Fischella, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Ukuzaji wa Uinjilishaji Mpya, aliizungumzia hija hii ,akisema, waamini zaidi 50, 000, walitarajiwa kushiriki katika hija hii hapo May 5 . Na kwamba ulikuwa ni wakati kwa waamini hao, kutafakari kwa namna nyepesi juu ya imani na uchaji uliosimikwa kwa kina, katika maisha ya kuziishi alama za kuonekana, kama kaburi la Mtakatifu Petro, zenye kukumbusha imani ya watu wa karne zilizopita na hivyo kuwa ushuhuda katika utamaduni wa imani, zenye kuhimiza na kutupatia mwamko na hamu ya kuuishi imani kwa shauku zaidi.

Askofu Mkuu Fischella alizitaja jumuiya hizi kuwa ni shuhuda hai mbalimbali kutoka kwa watu wa lika na hali mbalimbali wanaotafuta kuiimarisha na kuiishi imani yao si kwa maneno tu lakini katika utendaji wa maisha ya kila siku, katika umoja kamili wa kidini na kanisa.

Kati ya wanajumuiya waliokuwepo, ni kutoka Roma, ambao waliwasilisha mchoro maalum wa karne ya 13 unaomwonyesha Mama Bikira Maria na Mtoto wake, ili mchoro huo, upate mastahili ya kuwekwa Altareni. Sanamu hiyo iliyochorwa katika kipande cha ubao , na hujulikana kwa jina la Mama Yetu Asiyepungukiwa, wa Mazao, pia inaitwa kwa jina jingine, Mama Yetu wa Quintiliolo.








All the contents on this site are copyrighted ©.