2013-05-07 15:03:16

Rais wa Uswiss atembelea Vatican.


Baba Mtakatifu Fransisko, Jumatatu akiwa katika Jengo lake la Vatican, alitembelewa na Rais wa Uswisi, Bwana Ueli Maurer. Mazungumzo ya viongozi hao yalifanyika katika hali za urafiki na maelewano , na walilenga hasa katika utetezi wa haki za binadamu, malezi ya vijana na kukuza haki na amani.

RaisMaurer baada ya kukutana na Papa , pia alikwenda kukutana na Katibu wa Vatican, Kardinali Tarcisio Bertone, akiwepo pia, Askofu Mkuu Dominique Mamberti, katibu kwa Mahusiano na nchi zingine wa Vatican. Katika majadiliano yao, walikumbuka tukio la karne nyingi la huduma ya ulinzi kwa Papa , inayotolewa na vijana kutoka Uswiss. Vijana hao, kila mwaka hula upya kiapo cha kumlinda Papa .

Pia walizungumzia masuala ya kuimarisha zaidi uhusiano mzuri uliopo kati ya Jimbo Takatifu na Nchi ya Uswiss, wakisisitiza hasa uimarishaji wa ushirikiano kati ya Kanisa Katoliki na Serikali ya Uswiss.

Kisha walitazama masuala mengine ya kawaida, kama utetezi wa haki za binadama na heshima ya utu wa mtu, malezi ya vijana, na ushirikiano wa kimataifa katika kukuza haki na amani.









All the contents on this site are copyrighted ©.