2013-05-06 09:49:33

Dumuni katika umoja na wachungaji wenu - Papa Fransisko.


Jumapili, pamoja na mvua iliyokuwa ikinyesha, maelfu ya waamini, wengi wao wakiwa ni wanachama wa mashirika ya kazi za Kitume na sala, walimiminika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kuhudhuria Ibada ya Misa, iliyoongozwa na Papa Fransisko, katika mazingira ya 'Mwaka wa Imani.
Maelfu ya wanajumuiya hawa wa Kikanisa, wengi wao wakiwa wamevaa mavazi ya kijadi, kanzu ndefu na misalaba mikubwa ,walitoka mataifa mbalimbali hasa ya ulaya: Italia, Hispania, Malta, Ureno na Ireland,n.k.

Papa Fransisko, aliwasalimu na kuwashukuru kwa ushupavu wao wa kuja kwa wingi licha ya hali mvua kunyesha, huku akifurahia mchanganyiko wa rangi za miavuli walioyokuwa wameibeba, bendera na mabango na ishara nyingine nyingi.

Aliwaambia, katika maadhimisho ya mwaka huu wa Imani, Mapenzi ya kumcha Mungu , yanatuongoza katika kukiona kilicho muhimu zaidi , iwapo tunadumu ndani ya kanisa, tukiwa tumeshikamana ndani ya usharika kamili na wachungaji wetu, ambao ni mpuo wa hewa safi. Ni kukutana na kile kama ilivyokuwa wakati wa mwanzo wa Kanisa, uzoefu ambao kwa siku hizi utunaita "uamsho mpya "au maisha ya kuigundua upya imani".
Papa Fransisko katika homilia hii alilenga hasa katika mambo matatu, kuineza Injili, Kanisa na roho ya kitume, akisistiza kwamba mambo haya kamwe yasisahaulike ...

Wakati akielezea umuhimu wake, alifanya rejea kwa Papa Mstaafu Benedict XVI, aliyezindua Mwaka wa Imani, katika jinsi alivyoieleza kwa ufasaha roho ya kiinjili, kwamba yeye mwenyewe binafsi( Fransisko) aliguswa na maelezo hayo ya jinsi inavyotakiwa kuizingatia kwa makini upendo huu wa kumcha Mungu, kama hazina bora kuliko zote, fumbo la ajabu la kiroho , ambalo ni nafasi ya kukutana na Yesu Kristo.

Papa Francisko, aliwaalika wote waliokuwa wakimsikiliza kuwa na maamuzi thabiti, kuushinda udhaifu na kuruhusu jumuiya zao , kutumika kama kichocheo cha huduma za kujenga upendo thabiti zaidi kwa Kristo. Tangu mwanzo wa Karne za Kanisa , alisisitiza , jumuiya za kazi za kitume na sala, zimekuwa mhimili wa utakatifu kwa watu wa nyakati zote, walioyaishi maisha ya kawaida yenye unyenyekevu mkubwa na uhusiano wa karibu na Bwana.

Papa aliendelea kuzungumzia kipengere cha pili , akiilenga roho wa kikanisa , kw a mara nyingine tena akimnukuu Papa Benedict XVI, na waraka wa Maaskofu wa Amerika Kusini, hati yao ya ‘Aparecida' , ambamo mmefafanuliwa bayana kwamba, Uchaji kwa Mungu, ni njia halali ya kuishi imani na hisia zote kwamba sisi ni sehemu ya Kanisa.
Papa aliyakondolea machoa makutano na kuwaambia , “inapendeza , na ni upendo kwa Kanisa”. Alitoa mwaliko kwao wote, kwa kuwataka wakubali kuongozwa na Kanisa tangu katika ngazi ya chini , kiparokia, kijimbo na kuwa kweli kuwa pafu la Imani na maisha ya Kikristu.
Katika sehemu ya tatu ya hotuba yake Papa Francisko , alitaja jinsi ambavyo anatamani roho ya kimisionari iwe kigezo muhimu cha fadhila hususani katika utendaji wote wa jumuiya za kikanisa na mashirika ya kitume na sala, kati ya imani na tamaduni zao.








All the contents on this site are copyrighted ©.