2013-05-04 08:48:14

Baadhi ya waamini waandikwa kwenye orodha ya mchakato wa kutangazwa kuwa Wenyeheri


Baba Mtakatifu Francisko baada ya kukutana na kuzungumza na Kardinali Angelo Amato, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza waamini kuwa wenyeheri na watakatifu, ameridhia kwamba, baadhi ya miujiza na karama za kishujaa zilizooneshwa kutokana na sala na maombi ya Watumishi wa Mungu wafuatao, ziingizwe kwenye mchakato wa kutangazwa kuwa Wenyeheri na hatimaye, watakatifu kadiri ya kanuni na utaribu wa Kanisa Katoliki.

Mtumishi wa Mungu Maria Cristina wa Savoi kutoka Italia, aliyekuwa Malkia wa Visiwa vya Sicily; na kuishi kunako mwaka 1812 hadi mwaka 1836.

Mtumishi wa Mungu Maria Bolognesi, kutoka Italia, mwamini mlei aliyeishi kunako mwaka 1924 hadi mwaka 1980. Hawa wametambuliwa na Kanisa kutokana na miujiza iliyotendwa nao. Wafuatao Kanisa limetambua na kukiri karama za kishujaa zilizooneshwa na:

Mtumishi wa Mungu Joaquim Rosella Ferra, Padre wa Jimbo la Mallorca, Hispania na Mwanzilishi wa Shirika la Wamissionari wa Moyo Mtakatifu wa Yesu na Maria, aliyeishi kunako mwaka 1833 hadi mwaka 1909.

Na wa mwisho katika orodha hii ni Mtumishi wa Mungu Maria Theresa wa Mtakatifu Yosefu, kutoka Poland, mwanzilishi wa Shirika la Watawa Wakarmeli wa Mtoto Yesu, aliyeishi kunako mwaka 1885 hadi mwaka 1946.







All the contents on this site are copyrighted ©.