2013-04-30 09:32:14

Wanajeshi waasi wasalimisha silaha Sudan ya Kusini! Huu ni mwanzo mpya!


Askari wa zamani wapatao elfu tatu wamerudisha silaha walizokuwa wanazimiliki kinyume cha sheria mikononi mwa Serikali kama sehemu ya masharti ya kupata msamaha uliotolewa hivi karibuni na Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini. Hawa ni wanajeshi wa Kikosi cha Jeshi la Ukombozi Kusini mwa Sudan kilichoanzishwa wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Wachunguzi wa mambo wanasema, hii ni hatua muhimu katika kulinda na kudumisha amani na utulivu Sudan, mchakato ambao unaendelea kuimarishwa na viongozi wa Serikali ya Sudan Kongwe na Sudan ya Kusini katika majadiliano yaliyofanyika hivi karibuni.

Maboresho ya mahusiano kati ya nchi hizi mbili yanaanza kuonekana kwa watu kujisikia kuwa na amani pamoja na utulivu, mambo ambayo yatakuwa ni kikolezo cha uzalishaji na maendeleo endelevu.







All the contents on this site are copyrighted ©.