Siku ya Kimataifa kuenzi Maisha itaongozwa na Kaulimbiu: Tunasadiki Utakatifu wa Maisha
Tuna Imani na Utakatifu wa Maisha ni kaulimbiu itakayoongoza adhimisho la Siku ya
Kimataifa kwa ajili ya Injili ya Maisha (Evangelium Vitae), kama itakavyoandaliwa
na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjiishaji mpya.
Baraza hilo limeandaa
mkutano Roma tarehe 15 na 16 Juni 2013, unaotajwa kuwa wa muhimu, na kama nafasi
kwa waaamini kutoka pande zote za dunia , kwa pamoja, kuungana na Baba Mtakatifu
Francisko , kama kundi moja , kushuhudia thamani takatifu ya maisha: iwe kwa wazee,
wagonjwa, walioko kufani na hata wale ambao bado kuzaliw au wale wote wanaoteswa
daima maradhi ya kimwili na taabu zingine.
Inatumainiwa kwamba , tukio hili
litakuwa ni fursa ya kuenzi, kuimarisha na kutia moyo, wale wote ambao kwa ukarimu
na unyenyekevu wameyatolea maisha yao yote bila ya kujibakiza, kufuata nyanyo za Mchungaji
mwema, Yesu Kristu, kwa ajili ya kuwahudumia kihali, kisaikolojia na kiroho, wazee,
walemavu, wagonjwa, wasiozaliwa bado, walioko kufani na wanao kabilwa na mateso mengine.
Ni matumaini ya waandaaji wa tukio hili kwamba, watu wengi watakaokusanyika katika
Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya adhimisho la Siku ya Kimataifa
ya Utakatifu wa Maisha, itakuwa ni ushuhuda wa nguvu toka Roma kwa dunia, ukiieleza
dunia yote, ukweli wa ujumbe wa Kuokoa wa Yesu: "Nimekuja ili wawe na uzima, tena
uzima tele(Yn 10:10).
Habari zaidi juu ya tukio hli zinapatikani katika ukurasa
wa mtandano WWW.ANNUSFIDEI.VA.