2013-04-27 12:17:23

Papa Francisko anasali kwa ajili ya kuwaombea waliokumbwa na ajali mjini Dhaka, Bangaladesh


Baba Mtakatifu Francisko anawaalika watumiaji wa mitandao ya kijamii maarufu kama twitter kuungana naye kusali kwa ajili ya kuwaombea watu waliopatwa na ajali ya kuangukiwa jengo mjini Dhaka, Bangaladesh, ili Mwenyezi Mungu aweze kuwafariji na kuziimarisha familia zilizoguswa na msiba huu mkubwa.

Hivi karibuni jengo la kiwanda cha kutengeneza nguo mjini Dhaka liliporomoka na kusababisha vifo vya watu 332 na wengi kujeruhiswa vibaya. Jeshi la Polisi nchini Bangaladesh limekwisha watia mbaroni wakurugenzi wakuu wawili wa kiwanda hicho kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Idadi ya watu waliofariki inaweza kuongezeka maradufu kwani inasemekana kwamba, kuna watu ambao bado wamefukiwa na kifusi cha jengo lililoporomoka.







All the contents on this site are copyrighted ©.