2013-04-27 07:24:36

Papa awapongeza watanzania kwa kusherehekea miaka 49 ya Jamhuri ya Muungano


Baba Mtakatifu Francisko amemtumia salam za matashi mema Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, katika Maadhimisho ya Kumbu kumbu ya Miaka 49 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baba Mtakatifu anawatakia watanzania wote heri, baraka, amani, ustawi na maendeleo hasa wakati huu anapoanza utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Viongozi kadhaa kutoka Jumuiya ya Kimataifa wameungana na watanzania katika Maadhimisho ya Miaka 49 ya Muungano wa Tanzania. Kauli mbiu ambayo imeongoza Maadhimisho ya Mwaka huu ni "Amani, utulivu na maendeleo ni matokeo ya Muungano".







All the contents on this site are copyrighted ©.