Rais Andry Nirina Rajoelina wa Madagascar azuru Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, mapema Ijumaa hii alikutana na Rais wa Kipindi cha Mpito
wa Madagascar, Mheshimiwa Andry Nirina Rajoelina . Baadaye Rais huyo alikutana na
Katibu wa Vatican , Kardinali Tarcisio Bertone akiwepo pia Askofu Mkuu Domenique Mamberti
, Katibu wa Vatican, kwa ajili ya mahusiano na nchi zingine. Katika majadiliano
yao yaliyofanyka katika hali ya kirafiki, walitazama hasa mahusiano mazuri yaliyopo
kati ya Jimbo Takatifu na Jamhuri ya Madagascar, na hali zingine za kijamii hasa zinazogusa
kwa uchungu maisha ya kijamii katika taifa hilo. Kwa namna ya pekee , walitazama
madhara ya utumiaji wa nguvu za kijeshi na mbavu katika ufanikishaji wa demokrasia,
na uboreshaji wa hali za kiuchumi na ukarabati wa mahusiano mazuri ngazi ya kimataifa.
Pia umuhimu wa mchango wa Kanisa Katoliki Madagascar, katika udumishaji wa majadiliano
ya kitaifa na uwepo huduma msingi, kama Afya na Elimu.